Sunday, August 25, 2013

HATIMAYE SIMBA WAFANIKIWA KUPATA ITC ZA AMISI TAMBWE NA GILBERT KAZE - SASA KUKIPIGA DHIDI YA JKT OLJORO JUMATANO




MWENYEKITI wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, leo mchana amefanikisha upatikanaji wa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa wachezaji wawili wa klabu hiyo kutoka nchini Burundi -Amissi Tambwe na Gilbert Kaze.

Wachezaji hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya taifa ya Burundi (Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania iliyochezwa jana kutokana na kutokamlika kwa uhamisho huo, jambo lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji wenyewe, uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu.

Rage aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku na imechukua chini ya saa 24 kuweka kufanikisha suala hilo. Katika taarifa yake kwa wana Simba, Mbunge huyo wa Tabora Mjini alisema amelazimika kuingilia kati suala hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa Vitalo, klabu waliyotoka wachezaji hao hawakuwa mjni na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba.

"Kila walipokuwa wakipigiwa simu kwa takribani siku tatu mfululizo walikuwa wakisema kwamba wako milimani. Sasa hawa watu wa Burundi wakikwambia wako miliman wanamaanisha wameenda kijijini kwao. Kuongea kwa simu pekee kusingetosha na ndiyo Kamati ya Utendaji ya Simba iliomba niende mwenyewe Burundi ili suala hili liishe," alisema.

Hii ni mara ya pili kwa Rage, ambaye ana uzoefu wa kuongoza soka kwa zaidi ya miongo mitatu, kuingilia kati suala la uhamisho wa wachezaji wa kimataifa. Miaka miwili iliyopita, Mwenyekiti huyo alilazimika pia kusafiri kwenda nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kushughulikia uhamisho wa mchezaji Gervais Kago ambao nao ulikuwa na matatizo.

Kutokana na kupatikana kwa ITC hizo, Kaze na Tambwe sasa wataruhusiwa kucheza katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya JKT OIljoro ya Arusha iliyopangwa kufanyika Jumatano ijayo mjini Arusha. Klabu ya Simba tayari imewakatia wachezaji hao vibali vya kufanya kazi hapa nchini.

Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba, Joeph Owino na Abel Dhaira, walicheza katika mechi ya jana kutokana na kukamilisha taratibu zote za uhamisho na kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini.

Imetolewa na

Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

Saturday, August 10, 2013

SIMBA SC YAIFYATUA SC VILLA MABAO 4-1 UWANJA WA TAIFA KATIKA SIMBA DAY

Kiungo wa Simba, Amri Kihemba akimtoka beki wa Sports Club Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo., Simba imeshinda 4-1. (Picha na Habari Mseto Blog) 
 Kipa wa Sports Club Villa ya Uganda, Elungat Martins akiota mpira katika nyavu la lango lake baada ya mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki kuifungia timu yake bao la tatu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Tunda Man, akitumbuiza katika tamasha hilo.

Friday, August 2, 2013

HANS POPPE AWASUTA YANGA MCHANA KWEUPEEE KUHUSU OLOYA

Na Mahmoud Zubeiry MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba amezungumza na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Moses Oloya kumuuliza kuhusu kusaini kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC na amekanusha. “Nimetoka kuzungumza na Oloya sasa hivi, ameniambia hajasaini Yanga, sasa sijui hizo habari zinatoka wapi,”alisema Poppe alipozungumza na BIN ZUBEIRY leo kwa simu kutoka Ureno. Japokuwa gazeti moja leo limeandika Oloya ametua Dar es Salaam kusaini Yanga, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu mchezaji huyo bado yupo Vietnam.
Waongo; Hans Poppe amesema amezungumza na Oloya na amemuambia hajasaini Yanga SC
Ni kweli Yanga wanamtaka mchezaji huyo na vyanzo vinasema Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Yussuf Mehboob Manji ameipa Kamati ya Mashindano ya klabu, inayohusika na masuala ya usajili pia, fungu la kutosha ambalo ‘piga ua’ litatosha kumlainisha Oloya abadilie uamuzi wake. Aidha, inadaiwa tayari mazungumzo kati ya Yanga na Oloya yanaendelea na kuna makubaliano- kana kwamba mchezaji huyo mwenye kasi, nguvu na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira amekubali kuwapuuza Simba SC.   Simba SC imetenga nafasi katika usajili wake wa wachezaji wa kigeni na ipo tayari kumsubiri Oloya hata hadi Januari baada ya makubaliano ya kimsingi. Kiungo huyo mshambuliaji wa The Cranes, yaani ndege aina ya Korongo aliyezaliwa miaka 20 iliyopita anamaliza mkataba wake na Saigon Xuan Thanh ya Vietnam mwezi huu, Agosti na kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Hans Poppe atakuja Septemba.
Wamebebana; Oloya akiwa amembeba mshambuliaji wa Azam, Brian Umony. Je, atajiunga naye Ligi Kuu ya Bara msimu ujao?

Kwa sababu hiyo, Simba imepanga kusajili wachezaji wanne wa kigeni ambao ni Waganda, kipa Abbel Dhaira, beki Joseph Owino na Warundi wawili, mmoja beki na mwingine mshambuliaji, Amisi Tambwe.    
Wazi sasa ni wakati wa mpambano wa watani, kuwania saini ya mchezaji huyo aliyekwenda Vietnam akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010.
Katika usajili wake, Yanga ina nafasi mbili za wachezaji wa kigeni, sasa ikiwa na watatu ambao ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Didier Kavumbangu- wakati bado ipo kwenye mazungumzo na Mganda, Hamisi Kiiza aongeze Mkataba.
Wakati huo huo, habari zinasema, Yanga SC wana mpango wa kuleta kiungo mshambuliaji hodari kutoka Brazil. 
Kwa sasa Hans Poppe amekwenda Ureno kushughulikia mpango mmoja mzuri kwa mustakabali wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, ambao amekuwa akiupigania kwa muda sasa na maendeleo yake ni mazuri.(kwa hisani ya binzubeiry blogspot)

Thursday, August 1, 2013

MAN CITY KWELI BALAA, YAIFUMUA AC MILAN 5-3 KOMBE LA AUDI...ILIONGOZA 5-0 NDANI YA DAKIKA 35, IKALETA MZAHA IKATUNGULIWA TATU ZA FASTA

MANENO ya kocha Manuel Pellegrini kwamba ana safu kali ya ushambuliaji dunia nzima, yameanza kudhihirika taratibu baada ya timu yake, Manchester City kuvuna mvua ya mabao kwenye mechi ya Kombe la Audi leo Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.
Mabao matano ndani ya dakika 35, yameitotesha AC Milan iliyopambana na kurudisha hadi kulala kwa 5-3.
David Silva alifunga bao la kwanza dakika ya tatu, kufuatia kazi nzuri ya Stevan Jovetic, na Micah Richards na Aleksandar Kolarov wakaongeza mengine dakika ya 19 na 22 na Edin Dzeko akafunga mawili ndani ya dakika tatu.
Stephan El Shaarawy akafunga mawili na Andrea Petagna akafunga lingine katika mabao matatu ya Milan.
Goals galore: Manchester City beat AC Milan 5-3 in the semi-finals of the Audi Cup
Kapu la mabao: Manchester City imefiunga AC Milan 5-3 katika Nusu Fainali ya Kombe la Audi
Quick out the blocks: David Silva (right) gave Manchester City the lead in the third minute
David Silva (kulia) aliifungia la kwanza Manchester City
On target: Micah Richards doubled City's lead from close range in the 20th minute
Micah Richards akifunga la pili
Delight: Richards celebrates his goal with new signing Fernandinho at the Allianz Arena
Delight: Richards celebrates his goal with new signing Fernandinho at the Allianz Arena
Flying Serb: Aleksandar Kolarov drilled home Manchester City's third goal midway through the first half
Aleksandar Kolarov akiwafungia Manchester City la tatu
Rampant: Kolarov and Richards celebrate after City stormed into a 3-0 lead
Kolarov na Richards wakishangilia
At the double: Two goals in three minutes from Edin Dzeko extended City's lead to 5-0
Edin Dzeko alihitimisha karamu ya mabao ya City
Relaxed: Manuel Pellegrini looks content
Ametulia: Manuel Pellegrini akiangalia mechi
Unhappy: Goalkeeper Marco Amelia looks bemused
Hana furaha: kipa Marco Amelia akionekana aliyeudhika
At the double: Two goals in three minutes from Edin Dzeko extended City's lead to 5-0
Stephan El Shaarawy alifunga mawili kwa Milan
Back in it: Andrea Petagna slotted past Joe Hart in the 43rd minute as City led 5-3 at half-time

HIVI NDIVYO BAYERN MUNICH WALIVYOITUNGUA SAO PAOLO YA BRAZIL






JEURI YA PESA : Spurs wataka kuifanyia umafia Arsenal,wafikiria kutumbukiza mkono kwa Suarez


Wakati wa usajili kuna wengine huwa wanaachwa na maumivu na kuna wengine huwa wanamaliza kipindi hicho wakiwa wanacheka meno yote nje.
Sasa habari mbaya kwa Arsenal ni kwamba Tottenham wanaweza kuwafanyia umafia mahasimu wao hao wa London Kaskazini na kumchukua Luis Suarez kutoka Liverpool,kama Gareth Bale atakamilisha taratibu za kutua Real Madrid.
 
Tayari Madrid wameweka mezani paundi milioni 85 za kumtaka Bale japo mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy anaweka ngumu anataka paundi milioni 126.
Habari hizo zinaweza kuwa si nzuri kwa mashabiki wa Arsenal ambao wanaamini Suarez ataisaidia timu hiyo japo Liverpool bado wameweka ngumu kumuuza kwa dau la chini ya paundi milioni 50.

NAHODHA MWENGINE ADONDOKA UNYAMANI TAYARI KUDONDOKA MIAKA KADHAA KULISUKUMA GOZI MSIMBAZI

Taarifa zinaeleza nahodha na beki tegemeo wa timu ya taifa ya Burundi, Ingamba Murugamba, Kaze Gilbert maarufu kama Demunga amekubali kujiunga na Simba.
Demunga ambaye ni beki kitasa wa mabingwa wa Kombe la Kagame, Vital’O na Inhamba Murugamba, ameishaanza mazungumzo na SImba na huenda akaja nchini kusaini mkataba.

DEMUNGA AKIWA KAZINI
Demunga amekuwa gumzo kati ya mabeki waliofanya vizuri katika michuano ya Kagame iliyofanyika nchini Sudan.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zimeeleza kwa asilimia 90 ni kama tayari ameishatua katika klabu hiyo.
Kama itafanikiwa kumnasa, maana yake Simba itakuwa na manahodha wawili kutoka nchini Burundi.
Ilianza kumnasa mshambuliaji Amisi Tambwe ambaye ni nahodha wa Vital’O iliyotwaa Kombe la Kagame na akaibuka mfungaji bora na mchezaji bora wa michuano hiyo iliyofanyika Sudan

Lewandowski alianzisha tena,asema Dortmund wamemsaliti

Robert Lewandowski ameushambulia uongozi wa klabu yake ya Borussia Dortmund akisema ametendewa sivyo kuhusiana na matakwa yake ya kutaka kujiunga na Bayern Munich.

Makubaliano ya mshambuliaji huyo kutua Bayern Munich yameshindikana kwa Dortmund kumtaka amalize mkataba wake uliosalia mwaka mmoja na ataondoka bure.


Lewandowski alikuwemo kwenye kikosi cha Dortmund kilichoichapa maba0 4-2 Bayern kwenye German Super Cup.

Ilionekana ni kama masuala yake ya usajili wa kuhamia Bayern sasa yamefungwa rasmi lakini Lewandowski,ambaye alifunga mabao manne dhidi ya Real Madrid kwenye nusu fainali ya champions League msimu uliopita amelianzisha upya na anasema anahisi amesalitiwa na Dortmund.

Lewandowski anadai kuwa aliahidiwa Euro milioni 6 na bonasi kama atabaki kuelekea mwisho wa mkataba wake lakini jambo ambalo halijatekelezeka.

Mshambuliaji huyo alitua Dortmund akitokea Lech Poznan ya Poland mwaka 2010.

BYE BYE MUSSA MUDDE UNYAMANI


Simba imemalizana na aliyekuwa kiungo wake Mussa Mudde na sasa atarejea kwap Uganda ili aamue anakotaka kwenda.
“Tayari kila kitu kimeisha na Mudde, Simba tumeamua kuvunja mkataba na hilo lilikuwa ni wazo kutoka kamati ya ufundi baada ya Mganda huyu kushindwa kuonyesha kiwango,” kilieleza chanzo.
Lakini Simba pia kesho itakuwa na ugeni wa beki Joseh Owino, Mganda mwingine ambaye ilimuacha wakati akiwa mgonjwa.
Owino anatua nchini leo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuichezea Simba kwa mara nyingine.
Simba ilishaanza mazungumzo na Owino na wamekubaliana na sasa kinachosubiriwa ni mkataba huo ambao huenda wakaingia leo au kesho na kumtangaza rasmi kuwa mchezaji wake.

Simba ilianza kutamani kumrejesha tena beki huyo baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika mechi yake ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda ambayo aliichezea na ikashinda kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wiki iliyopita.

Simba yaunga mkono mechi za ligi kuu kuwa live Azam Tv

Wekundu wa Msimbazi Simba wameunga mkono mechi za ligi kuu soka Tanzania bara kuanzia msimu ujao kuoneshwa live na Azam Media kupitia kituo chake cha Televisheni cha Azam Tv.

Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuna faida kubwa mechi kuonekana moja kwa moja kwenye Televisheni kwahiyo wao kwa upande wao hawana sababu ya kukataa hilo lakini pia wakisema wanaamini linapokuja suala la kucheza uwanjani timu zote zipo sawa.
Mahasimu wa Simba kwenye soka la Tanzania Yanga Africa wenyewe wameweka ngumu mechi zao kuoneshwa live na Azam Tv wakisema wanataka kulipwa zaidi ya timu nyingine,lakini pia wakitia ngumu kwasababu Azam FC ni wapinzani wao wakubwa kwenye soka la Tanzania.

Azam Media wameingia mkataba wa awali wa kuonesha mechi za ligi kuu ya VodaCom kwa miaka mitatu wakimwaga kiasi cha shilingi bilioni 5.