Na Mahmoud Zubeiry
MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba
amezungumza na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Moses Oloya
kumuuliza kuhusu kusaini kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC na
amekanusha.
“Nimetoka
kuzungumza na Oloya sasa hivi, ameniambia hajasaini Yanga, sasa sijui
hizo habari zinatoka wapi,”alisema Poppe alipozungumza na BIN ZUBEIRY
leo kwa simu kutoka Ureno.
Japokuwa
gazeti moja leo limeandika Oloya ametua Dar es Salaam kusaini Yanga,
lakini BIN ZUBEIRY inafahamu mchezaji huyo bado yupo Vietnam.
Ni
kweli Yanga wanamtaka mchezaji huyo na vyanzo vinasema Mwenyekiti wa
klabu hiyo, Alhaj Yussuf Mehboob Manji ameipa Kamati ya Mashindano ya
klabu, inayohusika na masuala ya usajili pia, fungu la kutosha ambalo
‘piga ua’ litatosha kumlainisha Oloya abadilie uamuzi wake.
Aidha,
inadaiwa tayari mazungumzo kati ya Yanga na Oloya yanaendelea na kuna
makubaliano- kana kwamba mchezaji huyo mwenye kasi, nguvu na uwezo
mkubwa wa kumiliki mpira amekubali kuwapuuza Simba SC.
Simba
SC imetenga nafasi katika usajili wake wa wachezaji wa kigeni na ipo
tayari kumsubiri Oloya hata hadi Januari baada ya makubaliano ya
kimsingi.
Kiungo
huyo mshambuliaji wa The Cranes, yaani ndege aina ya Korongo
aliyezaliwa miaka 20 iliyopita anamaliza mkataba wake na Saigon Xuan
Thanh ya Vietnam mwezi huu, Agosti na kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati
ya Usajili ya Simba, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Hans Poppe atakuja Septemba.
Kwa sababu hiyo, Simba imepanga kusajili wachezaji wanne wa kigeni ambao ni Waganda, kipa Abbel Dhaira, beki Joseph Owino na Warundi wawili, mmoja beki na mwingine mshambuliaji, Amisi Tambwe.
Wazi sasa ni wakati wa mpambano wa watani, kuwania saini ya mchezaji huyo aliyekwenda Vietnam akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010.
Katika usajili wake, Yanga ina nafasi mbili za wachezaji wa kigeni, sasa ikiwa na watatu ambao ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Didier Kavumbangu- wakati bado ipo kwenye mazungumzo na Mganda, Hamisi Kiiza aongeze Mkataba.
Wakati huo huo, habari zinasema, Yanga SC wana mpango wa kuleta kiungo mshambuliaji hodari kutoka Brazil.
Kwa sasa Hans Poppe amekwenda Ureno kushughulikia mpango mmoja mzuri kwa mustakabali wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, ambao amekuwa akiupigania kwa muda sasa na maendeleo yake ni mazuri.(kwa hisani ya binzubeiry blogspot)
![]() |
Waongo; Hans Poppe amesema amezungumza na Oloya na amemuambia hajasaini Yanga SC |
![]() |
Wamebebana; Oloya akiwa amembeba mshambuliaji wa Azam, Brian Umony. Je, atajiunga naye Ligi Kuu ya Bara msimu ujao? |
Kwa sababu hiyo, Simba imepanga kusajili wachezaji wanne wa kigeni ambao ni Waganda, kipa Abbel Dhaira, beki Joseph Owino na Warundi wawili, mmoja beki na mwingine mshambuliaji, Amisi Tambwe.
Wazi sasa ni wakati wa mpambano wa watani, kuwania saini ya mchezaji huyo aliyekwenda Vietnam akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010.
Katika usajili wake, Yanga ina nafasi mbili za wachezaji wa kigeni, sasa ikiwa na watatu ambao ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Didier Kavumbangu- wakati bado ipo kwenye mazungumzo na Mganda, Hamisi Kiiza aongeze Mkataba.
Wakati huo huo, habari zinasema, Yanga SC wana mpango wa kuleta kiungo mshambuliaji hodari kutoka Brazil.
Kwa sasa Hans Poppe amekwenda Ureno kushughulikia mpango mmoja mzuri kwa mustakabali wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, ambao amekuwa akiupigania kwa muda sasa na maendeleo yake ni mazuri.(kwa hisani ya binzubeiry blogspot)
No comments:
Post a Comment