MANENO ya kocha Manuel Pellegrini kwamba
ana safu kali ya ushambuliaji dunia nzima, yameanza kudhihirika
taratibu baada ya timu yake, Manchester City kuvuna mvua ya mabao kwenye
mechi ya Kombe la Audi leo Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.
Mabao matano ndani ya dakika 35, yameitotesha AC Milan iliyopambana na kurudisha hadi kulala kwa 5-3.
David Silva alifunga bao la kwanza
dakika ya tatu, kufuatia kazi nzuri ya Stevan Jovetic, na Micah Richards
na Aleksandar Kolarov wakaongeza mengine dakika ya 19 na 22 na Edin
Dzeko akafunga mawili ndani ya dakika tatu.
Stephan El Shaarawy akafunga mawili na Andrea Petagna akafunga lingine katika mabao matatu ya Milan.

Kapu la mabao: Manchester City imefiunga AC Milan 5-3 katika Nusu Fainali ya Kombe la Audi

David Silva (kulia) aliifungia la kwanza Manchester City

Micah Richards akifunga la pili

Delight: Richards celebrates his goal with new signing Fernandinho at the Allianz Arena

Aleksandar Kolarov akiwafungia Manchester City la tatu

Kolarov na Richards wakishangilia

Edin Dzeko alihitimisha karamu ya mabao ya City

Ametulia: Manuel Pellegrini akiangalia mechi

Hana furaha: kipa Marco Amelia akionekana aliyeudhika

Stephan El Shaarawy alifunga mawili kwa Milan

No comments:
Post a Comment