Saturday, July 20, 2013

Okwi, Patrick Ochan waomba kurudi Simba


.
Ochan, kiungo aliyeuzwa na Simba kwenda TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kiasi cha dola 100,000  anataka kurudi Msimbazi haraka iwezekanavyo kwa uhamisho wa mkopo baada ya kuchoshwa na maisha ya Lubumbashi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Ochan mwenye umri wa miaka 27, ameonyeshwa kukerwa na lundo la wachezaji mahiri na wasio mahiri ndani ya TP Mazembe ambalo limesababisha akose namba ya kudumu klabu hapo.
“Nataka kurudi Simba kwa mkopo, nimechoshwa na maisha ya Mazembe. Tajiri (Moise Katumbi) anarundika wachezaji wengi hapa na nafasi ya kucheza imekuwa ngumu. Waambie watu wa Simba nataka kurudi klabuni kwangu kwa mkopo. Mwambie Kaburu (Geofrey-aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba) nataka kurudi Simba,” alisema Ochan.
Ochan amekiri kwamba mara kadhaa amejaribu kuihama Mazembe ikiwemo kutaka kutimkia Afrika Kusini kuichezea timu ya Golden Arrows, lakini Katumbi ametia ngumu.
“Kuhama kwa mkopo inawezekana. Nitazungumza na viongozi huku nadhani inawezekana kabisa kwa sababu watataka nipate muda wa kucheza. Baada ya wiki mbili nitakuja Uganda. Kwa kweli nataka kurudi zangu Simba,” alisema Ochan ambaye aliuzwa pamoja na Mbwana Samata wakitokea Simba.
Katika hatua nyingine, Emmanuel Okwi naye amempigia simu mmoja ya viongozi wa Simba na kuomba arudi Msimbazi.
Okwi, ambaye yupo jijini Kampala akiwa amesusa kwenda Etoile du Sahel kwa mwezi moja sasa, ameomba kurudi Simba kwa madai kuwa amekuwa hapewi nafasi ya kucheza, lakini mbaya zaidi amekuwa halipwi mshahara na hajamaliziwa fedha zake za kusaini mkataba wa miaka mitatu.
“Ni kweli amepiga simu kuomba tumrudishe Simba, lakini tukifanya hivyo tutakosa Sh 480 milioni ambazo tunawadai Etoile,”alisema kiongozi mmoja wa Simba. Kiongozi huyo alisema kinachoweza kufanyika ni klabu hiyo ya Tunisia angalau iwalipe Sh 300 milioni halafu Okwi aje Simba kucheza kwa mkopo.
Mwanaspoti ilimtafuta Okwi kwa simu jana Ijumaa, lakini simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila kupokewa.(kwa hisani ya MWANASPOT)

BARCELONA WAIKATA MAINI MAN UNITED, WAIAMBIA ISAHAU KABISA KUHUSU FABREGAS

KLABU ya Barcelona imeiambia Manchester United isahau kumsaini Cesc Fabregas.
Huku United wakiendelea kuibania Chelsea kwa Wayne Rooney, wanakutana na hali kama hiyo kwa Barcelona ambao wanasema hawawezi kumuuza nyota wao huyo.
Ikiwa tayari imepiga chini ofa ya United ya Pauni Milioni 26 kwa ajili ya kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania, Makamu wa Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema: "Barca haitakaribisha ofa yoyote juu ya Cesc. Hahamishwi.’
Optimist: David Moyes is hopeful over a transfer move for Cesc Fabregas
Mbishi: David Moyes anatumai kumnasa Cesc Fabregas
Top target: Manchester United are keen to capture Cesc Fabregas after missing out on Thiago to Bayern
Mlengwa Mkuu: Manchester United inamtaka sana Cesc Fabregas baada ya kumkosa Thiago aliyetimkia Bayern
 
United wanaendelea kukomaa na nia ya kumsajili Fabregas kwa sababu wanaamini anataka kuondoka Nou Camp.
Wakati Mtendaji Mkuu, Ed Woodward alirejea Uingereza kushughulikia dili hilo, kocha Moyes aliweka wazi kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Sydney mapema leo.
"Mtendaji Mkuu amekuwa akishughulikia suala hilo sasa na nipo kwenye mawasiliano naye. Natumai kufahamu zaidi siku ijayo. Nitapata taarifa zaidi juu ya mambo yanavyoendelea siku ijayo,"alisema.
Pamoja na hayo, Arsene Wenger pia bado anajiamini kwamba Fabregas atarejea Emirates akiamua kuondoka Barcelona.
Kiungo huyo amewaambia rafiki zake wa karibu London na Barcelona kwamba atarejea Ligi Kuu England tu kuchezea Arsenal, hali ambayo inavunja matumaini ya Moyes kumpata Mspanyola huyo. 
Arsenal wanajua Fabregas atabakia kwa angalau miezi 12 mingine, lakini ikiwa kuna mabadiliko, The Gunners wapo nafasi ya mbele kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kwa Pauni Milioni 25.
United inaendelea pia kumfukuzia Gareth Bale, winga wa Tottenham ambaye pia anatakiwa na Real Madrid. Moyes pia ni shabiki wa mchezaji wa Real, Luka Modric. Anahitaji viungo kuimarisha timu yake.

CHAMA LA WANA LAMALIZA MKUTANO SALAMA SALMINI

clip_image001Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa Simba wa kujadili maendeleo ya klabu hiyo ulioanza saa nne kamili asubuhi na kumalizika saa tano kamili katika Bwalo la Maofisa wa Polisi jijini Dar es Salaam leo, ambapo wanachama zaidi ya 700 walihudhuria mkutano huo.
Mwanachama wa Simba kutoka Iringa akiuliza swali katika mkutano huo.Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali (kushoto) akifuatilia mkutano huo.Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano huo.Wanachama wa Simba wakimpongeza Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.Wanachama wa Simba wakionyesha furaja yao kwa Mwenyekiti wao baada ya mkutano kumalizika.Tuko pamoja Mwenyekiti.....Hongera sana.....Kila mwanachama alikuwa na shauku ya kutaka kusalimiana na Rage baada ya kufunga rasmi Mkutano Mkuu wa Simba leo asubuhi.Asanteni sana, hapa Rage anaonekana kama akisema.Rage akisamiliana na Mwenyekiti wa zamani wa Simba Hassan Dalali baada ya kumalizika kwa mkutano.Rage akitoka katika ukumbi wa mkutano.Wanachama wa Simba wakimpongeza Rage baada ya kufunga rasmi mkutano Mkuu wa kujadili maendeleo ya klabu hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Saturday, July 13, 2013

WENGER AANZA MAZUNGUMZO YA KUONGEZA MKATABA MPYA ARSENAL

KOCHA Arsene Wenger yu mbioni kurefusha muda wake wa kuendelea kufanya kazi Arsenal, baada ya kugundulika ameanza mazungumzo ya Mkataba mpya na klabu.
Mkataba wa sasa wa Mfaransa huyo unaisha majira yajayo ya joto, na ikazua tetesi huenda huo ukawa mwisho wake wa kufanya kazi katika klabu hiyo.
Lakini Wenger amesema nia yake ni kuongeza Mkataba wa mshahara wa Pauni Milioni 7.5 kwa msimu na mazungumzo ya awali na Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis yanaendelea.
Signing on: Arsene Wenger is set to seal a new deal at the Emirates and snub suitors PSG
Saini hapa: Arsene Wenger anajiandaa kusaini Mkataba mpya Emirates na kuzima ndoto za kuhamia PSG
Signing on: Arsene Wenger is set to seal a new deal at the Emirates and snub suitors PSG
Staying put: Arsene Wenger (left) will stay at Arsenal after admitting talks over a new deal have begun
Anabaki: Arsene Wenger (kushoto) atabaki Arsenal baada ya kusema mazungumzo ya Mkataba mpya yameanza.
Lads on tour: Jack Wilshere and his Arsenal team-mates arrived in Indonesia to start the pre-season tour
Jack Wilshere na wachezaji wenzake wa Arsenal wamewasili Indonesia kuanza ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya
Men of many talents: Alex Oxlade-Chamberlain showed his skills on the piano
Vipaji vilivyojificha: Alex Oxlade-Chamberlain (juu) na Wojciech Szczesny wakionyesha vuipaji vyao vya kupiga piano 
Men of many talents: Wojciech Szczesny showed his skills on the piano
"Kuhusishwa na PSG kupo kwa sababu mimi ni Mfaransa na ninawajua wamiliki. Lakini kama hiyo ndiyo sababu ningekuwa huko tayari.
"Moyo wangu upo na Arsenal. Mimi si PSG kwa sababu moyo wangu upo na Arsenal,"alisema. 
Wenger amewasili Indonesia jana kwa ajili ya mechi ya kwanza ya ziara ya Arsenal Mashariki ya Mbali akiwa na mshambuliaji kinda wa miaka 20, Mfaransa Yaya Sanogo, kutoka Auxerre, mchezaji pekee aliyemsajili hadi sasa majira haya ya joto.
Baada ya miaka kadhaa ya ubakhili, The Gunners itakuwa tayari kubomoa benki sasa kusajili japo mchezaji mmoja wa bei kubwa.
Wenger anaweza kufanikisha usajili wa Pauni Milioni 23 wa mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, wakati klabu hiyo pia inawataka Wayne Rooney na Luis Suarez.

HAYA SASA KAAENI TAYARI KWA MASHUTI YA MBALI,AMIS TAMBWE TAYAAAAAARI SIMBA


Mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na Wekundu wa Msimbazi Simba Amissi Tambwe ndio imekuwa gumzo la usajili kwa wekundu hao baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili hapo jana.

Tambwe ametua akitokea Vital’O,ya Burundi na ametupia wavuni mabao 18 kwenye msimu uliopita na kunyakuwa kiatu cha dhahabu kwenye ligi ya Burundi.

Mshambuliaji huyo ameibuka pia mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa Africa mashariki na kati maarufu kombe la Kagame,michuano iliyomalizika huko Sudan kwa Vital'o kuibuka na ubingwa.
         Karibu Tanzania mimi ndio Zakharia Hanspope

Tambwe ambaye ndiye mshambuliaji chaguo la kwanza kwenye timu ya Taifa ya Burundi Inthamba Murugamba amekuwa mchezaji wa nne raia wa kigeni kwa msimu huu kutua Simba huku wengine wakiwa bado wanasotea kusajiliwa wakiwemo Mganda Assumani Buyinza,Samuel Ssenkoomi, MCongo Felix Cuipo na James Kun kutoka Sudan Kusini.

Saturday, July 6, 2013

MKUTANO MKUU SIMBA SC KUFANYIKA JULAI 20 POLISI

Mkutano Mkuu pia utajadili suala la Kaburu (kushoto). Katikati ni Mwenyekiti wa klabu, Alhaj Ismail Aden Rage na kulia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Popope.

MKUTANO Mkuu wa mwaka wa klabu ya Simba SC, utafanyika Julai 20, mwaka huu katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oystrebay, Dar es Salaam. Kaimu Makamu Mwenyekiti wa S.S.C., Joseph Itang’are ‘Kinesi’ ameiambia mpiramaendeleo asubuhi ya leo kwamba, uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji, kilichofanyika kwa siku mbili mfululizo Dar es Salaam na kufikia tamati jana. Kinesi, anayekaimu nafasi ya Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyejiuzulu miezi mitatu iliyopita, alisema kwamba kwa sasa wapo katika maandalizi ya Mkutano huo wa Kikatiba. Pamoja na kupokea taarifa za msingi za klabu kwa mwaka mzima, Mkutano huo pia utajadili ombi la kujiuzulu kwa Kaburu, ambalo tayari limepata baraka za Kamati ya Utendaji. Lakini Kaburu anaonekana kama kujutia uamuzi wake na katika siku za karibuni amekuwa karibu mno na timu sambamba na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo suala la usajili. Pamoja na kuamua kuhusu Mkutano Mkuu, Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba kilipitisha suala la kuongezewa Mikataba kwa Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Ofisa Habari wa klabu, Ezekiel Kamwaga. Kikao hicho pia kiliidhinisha kiungo Kiggi Makassy kwenda kutibiwa nchini India kufuatia kuumia katikati ya msimu uliopita akiichezea Simba SC mchezo wa kirafiki dhidi ya CDA mjini Dodoma. Taarifa ya Simba SC jana ilisema kwamba kwa sasa klabu hiyo inapanga ahadi na hospitali nchini India kwa ajili ya mchezaji huyo kwenda huko kutibiwa. Kiggi aliumia akiwa katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka mahasimu, Yanga SC na jithada za kumponya kwa tiba za wataalamu wa nchini zimegonga mwamba na sasa anasogezwa mbele. Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba, Simba SC inatarajia kuwa na wiki ya kijamii kuanzia Agosti 5 hadi 11, mwaka huu kuelekea tamasha la kuazimisha siku ya klabu ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day. Katika wiki hiyo, mabingwa hao wa zamani wa Bara watatembelea kituo cha watoto yatima na kuwafariji kwa misaada, watatembelea wagonjwa, watahudhuria kozi maalum iliyoandaliwa na wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro, watatembelea shule kuhamasisha watoto kupenda soka na hususan klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, watatembelea vyombo vya habari kuimarisha uhusiano na kufanya ibada maalum klabuni kwao, kuwarehemu wachezaji, viongzi, wanachama na wapenzi wa tmu hiyo waliotangulia mbele ya haki na kujiombea mema siku zijazo.  Katika hatua nyingine, Simba SC imesema Chuo Kikuu Huria kimekwishawakabidhi makabrasha ya awali ya Mpango Mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo na Kamati ya Utendaji itakutana Julai 13 kuipitia, kabla ya kuirejesha kwa watalaamu wao hao ili ikamilishwe tayari kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama kwa hatua zaidi.

Thursday, July 4, 2013

TANZANIA WAKABIDHIWA RASMI UWANJA WA TAIFA NA WACHINA

 Balozi wa China, Lu Youqung akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga na Balozi wa China, Lu Youqung wakati wa hafla ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa.
Balozi wa China, Lu Youqung  akimkabidhi ufunguo Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara kama ishara ya makabidhiano rasmi ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
PICHA ZOTE NA HABARI MSETO BLOG

RYAN GIGGS ATEULIWA KOCHA/MCHEZAJI MANCHESTER UNITED

Klabu ya Manchester United leo imemtangaza mchezaji mkongwe zaidi wa klabu hiyo kuwa kocha wakati akiwa bado anaendelea kuichezea klabu hiyo.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mtandao rasmi wa Manchester United kwamba Giggs ambaye hivi karibuni alimaliza mafunzo yake ya ukocha atakuwa mmoja ya jopo la makocha watakaomsaidia David Moyes kuendesha jahazi liloachwa na Sir Alex Ferguson.

Pia wakati huo huo kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba David Moyes amemteua Phil Neville kuwa kocha wa timu ya kwanza.

SIMBA SC KUPIGA KAMBI KENYA NA KUSHIRIKI MICHUANO MAALUMU YA KILIMO, KIGGI MAKASY HUYOOOOO KUTIBIWA INDIA


WAKATI Simba SC imealikwa kushiriki michunao ya Kilimo mjini Kisumu, Kenya, kiungo wake Kiggi Makassy atakwenda kutibiwa nchini India kufuatia kuumia katikati ya msimu uliopita akiichezea Simba SC mchezo wa kirafiki dhidi ya CDA mjini Dodoma. Taarifa ya Simba SC, imesema kwamba kwa sasa klabu hiyo inapanga ahadi na hospitali nchini India kwa ajili ya mchezaji huyo kwenda huko kutibiwa.

Kiggi aliumia akiwa katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka mahasimu, Yanga SC na jithada za kumponya kwa tiba za wataalamu wa nchini zimegonga mwamba na sasa anasogezwa mbele. Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba, Simba SC inatarajia kuwa na wiki ya kijamii kuanzia Agosti 5 hadi 11, mwaka huu kuelekea tamasha la kuazimisha siku ya klabu ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day. Katika wiki hiyo, mabingwa hao wa zamani wa Bara watatembelea kituo cha watoto yatima na kuwafariji kwa misaada, watatembelea wagonjwa, watahudhuria kozi maalum iliyoandaliwa na wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro, watatembelea shule kuhamasisha watoto kupenda soka na hususan klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, watatembelea vyombo vya habari kuimarisha uhusiano na kufanya ibada maalum klabuni kwao, kuwarehemu wachezaji, viongzi, wanachama na wapenzi wa tmu hiyo waliotangulia mbele ya haki na kujiombea mema siku zijazo.  Katika hatua nyingine, Simba SC imesema Chuo Kikuu Huria kimekwishawakabidhi makabrasha ya awali ya Mpango Mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo na Kamati ya Utendaji itakutana Julai 13 kuipitia, kabla ya kuirejesha kwa watalaamu wao hao ili ikamilishwe tayari kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama kwa hatua zaidi. Simba pia itafanya ziara Katavi mkoani Rukwa, kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  kucheza mechi ya kirafiki na itaondoka Dar es Salaam Julai 13 na baada ya hapo itaelekea kucheza mechi za kirafiki Tabora, Mwanza na Mara kabla ya kuweka kambi fupi Kenya na baadae kushiriki mashindano ya Kilimo yatakayofanyika Kisumu Kenya kuanzia Julai 31 hadi Agosti 4.  Wakati huo huo:  Simba B inatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam  kwenda Arusha kwa ajili ya michuano ya Kombe la Rolingstone inayotarajiwa kuanza Julai 6, 2013.