KLABU ya Barcelona imeiambia Manchester United isahau kumsaini Cesc Fabregas.
Huku United wakiendelea kuibania Chelsea
kwa Wayne Rooney, wanakutana na hali kama hiyo kwa Barcelona ambao
wanasema hawawezi kumuuza nyota wao huyo.
Ikiwa tayari imepiga chini ofa ya United
ya Pauni Milioni 26 kwa ajili ya kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania,
Makamu wa Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema: "Barca
haitakaribisha ofa yoyote juu ya Cesc. Hahamishwi.’

Mbishi: David Moyes anatumai kumnasa Cesc Fabregas

Mlengwa Mkuu: Manchester United inamtaka sana Cesc Fabregas baada ya kumkosa Thiago aliyetimkia Bayern
United wanaendelea kukomaa na nia ya kumsajili Fabregas kwa sababu wanaamini anataka kuondoka Nou Camp.
Wakati Mtendaji Mkuu, Ed Woodward
alirejea Uingereza kushughulikia dili hilo, kocha Moyes aliweka wazi
kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Sydney mapema leo.
"Mtendaji Mkuu amekuwa akishughulikia suala hilo sasa na nipo kwenye mawasiliano naye. Natumai kufahamu zaidi siku ijayo. Nitapata taarifa zaidi juu ya mambo yanavyoendelea siku ijayo,"alisema.
Pamoja na hayo, Arsene Wenger pia bado anajiamini kwamba Fabregas atarejea Emirates akiamua kuondoka Barcelona.
Kiungo huyo amewaambia rafiki zake wa
karibu London na Barcelona kwamba atarejea Ligi Kuu England tu kuchezea
Arsenal, hali ambayo inavunja matumaini ya Moyes kumpata Mspanyola
huyo.
Arsenal wanajua Fabregas atabakia kwa
angalau miezi 12 mingine, lakini ikiwa kuna mabadiliko, The Gunners wapo
nafasi ya mbele kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, kwa
Pauni Milioni 25.
United inaendelea pia kumfukuzia Gareth
Bale, winga wa Tottenham ambaye pia anatakiwa na Real Madrid. Moyes pia
ni shabiki wa mchezaji wa Real, Luka Modric. Anahitaji viungo kuimarisha
timu yake.
No comments:
Post a Comment