KOCHA Arsene Wenger yu mbioni kurefusha
muda wake wa kuendelea kufanya kazi Arsenal, baada ya kugundulika
ameanza mazungumzo ya Mkataba mpya na klabu.
Mkataba wa sasa wa Mfaransa huyo unaisha
majira yajayo ya joto, na ikazua tetesi huenda huo ukawa mwisho wake wa
kufanya kazi katika klabu hiyo.
Lakini Wenger amesema nia yake ni
kuongeza Mkataba wa mshahara wa Pauni Milioni 7.5 kwa msimu na
mazungumzo ya awali na Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis yanaendelea.

Saini hapa: Arsene Wenger anajiandaa kusaini Mkataba mpya Emirates na kuzima ndoto za kuhamia PSG


Anabaki: Arsene Wenger (kushoto) atabaki Arsenal baada ya kusema mazungumzo ya Mkataba mpya yameanza.

Jack Wilshere na wachezaji wenzake wa Arsenal wamewasili Indonesia kuanza ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya

Vipaji vilivyojificha: Alex Oxlade-Chamberlain (juu) na Wojciech Szczesny wakionyesha vuipaji vyao vya kupiga piano

"Kuhusishwa na PSG kupo kwa sababu mimi ni Mfaransa na ninawajua wamiliki. Lakini kama hiyo ndiyo sababu ningekuwa huko tayari.
"Moyo wangu upo na Arsenal. Mimi si PSG kwa sababu moyo wangu upo na Arsenal,"alisema.
Wenger amewasili Indonesia jana kwa
ajili ya mechi ya kwanza ya ziara ya Arsenal Mashariki ya Mbali akiwa na
mshambuliaji kinda wa miaka 20, Mfaransa Yaya Sanogo, kutoka Auxerre,
mchezaji pekee aliyemsajili hadi sasa majira haya ya joto.
Baada ya miaka kadhaa ya ubakhili, The Gunners itakuwa tayari kubomoa benki sasa kusajili japo mchezaji mmoja wa bei kubwa.
Wenger anaweza kufanikisha usajili wa
Pauni Milioni 23 wa mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, wakati
klabu hiyo pia inawataka Wayne Rooney na Luis Suarez.
No comments:
Post a Comment