WAKATI
Simba SC imealikwa kushiriki michunao ya Kilimo mjini Kisumu, Kenya,
kiungo wake Kiggi Makassy atakwenda kutibiwa nchini India kufuatia
kuumia katikati ya msimu uliopita akiichezea Simba SC mchezo wa kirafiki
dhidi ya CDA mjini Dodoma.
Taarifa
ya Simba SC, imesema kwamba kwa sasa klabu hiyo inapanga ahadi na
hospitali nchini India kwa ajili ya mchezaji huyo kwenda huko kutibiwa.
Kiggi
aliumia akiwa katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka
mahasimu, Yanga SC na jithada za kumponya kwa tiba za wataalamu wa
nchini zimegonga mwamba na sasa anasogezwa mbele.
Aidha,
taarifa hiyo imesema kwamba, Simba SC inatarajia kuwa na wiki ya
kijamii kuanzia Agosti 5 hadi 11, mwaka huu kuelekea tamasha la
kuazimisha siku ya klabu ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day.
Katika
wiki hiyo, mabingwa hao wa zamani wa Bara watatembelea kituo cha watoto
yatima na kuwafariji kwa misaada, watatembelea wagonjwa, watahudhuria
kozi maalum iliyoandaliwa na wadhamini wao, Bia ya Kilimanjaro,
watatembelea shule kuhamasisha watoto kupenda soka na hususan klabu hiyo
ya Mtaa wa Msimbazi, watatembelea vyombo vya habari kuimarisha uhusiano
na kufanya ibada maalum klabuni kwao, kuwarehemu wachezaji, viongzi,
wanachama na wapenzi wa tmu hiyo waliotangulia mbele ya haki na
kujiombea mema siku zijazo.
Katika
hatua nyingine, Simba SC imesema Chuo Kikuu Huria kimekwishawakabidhi
makabrasha ya awali ya Mpango Mkakati wa maendeleo ya klabu hiyo na
Kamati ya Utendaji itakutana Julai 13 kuipitia, kabla ya kuirejesha kwa
watalaamu wao hao ili ikamilishwe tayari kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu
wa wanachama kwa hatua zaidi.
Simba
pia itafanya ziara Katavi mkoani Rukwa, kwa mwaliko wa Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kucheza mechi ya kirafiki na itaondoka Dar es Salaam
Julai 13 na baada ya hapo itaelekea kucheza mechi za kirafiki Tabora,
Mwanza na Mara kabla ya kuweka kambi fupi Kenya na baadae kushiriki
mashindano ya Kilimo yatakayofanyika Kisumu Kenya kuanzia Julai 31 hadi
Agosti 4.
Wakati
huo huo: Simba B inatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda
Arusha kwa ajili ya michuano ya Kombe la Rolingstone inayotarajiwa
kuanza Julai 6, 2013.
No comments:
Post a Comment