Tuesday, June 18, 2013

ARSENAL KUMALIZANA NA HIGUAIN WIKI HII, KUSAJILI PIA KINDA LA U-21 YA HISPANIA LINALOITOA UDENDA NA REAL MADRID

KLABU ya Arsenal inatumai kumaliza miaka tisa ya kusubiri saini ya Gonzalo Higuain wiki hii kwa kuweka rekodi ya dau lake la usajili, Pauni Milioni 22 ofa waliyotoa kumnasa mshambuliaji huyo.
BIN ZUBEIRY inafahamu Muargentina huyo amekubali kuhamia Emirates majira haya ya joto na The Gunners - ambao pia wanaamini watambakiza beki Bacary Sagna na Laurent Koscielny kuelekea msimu ujao - wiki hii itafanya mipango rasmi ya kumsaini nyota huyo wa Real Madrid, ambaye ameambiwa yuko huru kuondoka Bernebeu.
On target: Real Madrid striker Gonzalo Higuain could become Arsenal's record signing in a £22m deal
Anatakiwa: Mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain anaweza kuibuka mchezaji ghali kuwahia kusajiliwa Arsenal, kwa Pauni Milioni 22
Watchful eyes: Arsenal boss Arsene Wenger has been reluctant to splash out hefty fees for players in the past
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yuko tayari kumwaga fedha kusajili

Mazungumzo baina ya viongozi wa Arsenal na wawakilishi wa Higuain yanaendelea vizuri na inasemekana kilichobaki ni klabu hizo mbili kukubaliana.
Kwa sasa dau kubwa la usajili walilowahi kutoa ni Pauni Milioni 15 kwa Zenit St Petersburg kumsajili Andrey Arshavin, Arsenal iko tayari kumpa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki Higuain.
The Gunners imekuwa ikimmezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 tangu akiwa River Plate, timu yake ya kwanza mwaka 2004.
Flop: The disappointing £15m capture of Andrey Arshavin is Arsenal's current record transfer fee
Amechuja: Andrey Arshavin amechemsha Arsenal licha ya kushikilia rekodi ya kusajiliwa bei mbaya

Arsenal ilijaribu uwezekano wa kumsajili Muargentina huyo mzaliwa wa Ufaransa mwaka 2006, lakini wakazidiwa kete na Real Madrid.
Lakini Wenger anatarajiwa kukata kiu yake ya muda mrefu kwa mshambuliaji huyo, Higuain hivi karibuni.
Arsenal imeendelea na nia yake thabiti ya kutaka kuwasajili  Wayne Rooney na Stevan Jovetic, lakini dili la Higuain ndilo la ukweli zaidi.
Young Gun? Arsenal are also lining up a move for Spanish U21 star Asier Illarramendi (centre)
Mtutu mdogo? Arsenal pia inataka kumsajili mchezaji wa U21 ya Hispania, Asier Illarramendi (katikati)
Wakati huo huo, The Gunners wanaongoza mbio ya kuwania saini ya nyota wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Hispania, Asier Illarramendi. 
Kiungo huyo wa ulinzi wa Real Sociedad mwenye thamani ya Pauni Milioni 10 anang'ara kwa sasa na anaitoa udenda na Real Madrid pia. 
Arsenal pia inamfuatilia Gilbert Imbula - lakini Illaramendi akuwa sahihi zaidi akicheza na Mikel Arteta.

Monday, June 17, 2013

WACHEZAJI WAKALI WA SOKA MAPUMZIKONI FUKWELI

 Portuguese midfielder Raul Meireles and his wife Ivone enjoy a stroll down the beach in Miami

Meireles alionyesha kifua chake kilichojaa tattoo akiwa na mkewe ufukweli huko Miami, Gerrards ufukweni Ibiza na Beckham arejea kazini Uchina

Baada ya msimu mgumu wa soka kote duniani, wachezaji wa soka duniani wamekuwa katika msimu wa mapumziko ya kiangazi.

Rockersports kupitia mtandao wa Sportsmail inaendelea kukupatia hatua za mapumziko ya wachezaji hao kutoka Las Vegas, mpaka Dubai, Ibiza na kurejea Las Vegas kila siku fuatilia.
 
RAUL MEIRELES (MIAMI)
Kiungo wa kireno Meireles ameonekana akivinjari huku akiuanika mwili wake uliojaa tatoo juani katika pwani ya Miami akiwa na mpenzi wake Ivone ambaye naye mwili wake umejaa mitatoo.

Meireles alielekea England mwaka 2010 alipojiunga na Liverpool akitokea Porto ya Ureno. Baadaye alijiunga na Chelsea na kujiunga na meneja wake wa zamani alipokuwa Porto Andre Villas-Boas.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 baadaye akajiunga na Fenerbahce ya Uturuki msimu uliopita kwa uhamisho wa pauni milioni £8 ambapo aliungana na nyota mwenzake katika klabu ya Liverpool  Dirk Kuyt.
Portuguese midfielder Raul Meireles and his wife Ivone enjoy a stroll down the beach in Miami
Kiungo mreno Raul Meireles akiwa na mkewe Ivone ndani ya ufukwe ya Miami 

Body art: Ivone Meireles shows off her tattoos
 Ivone Meireles akionyesha tattoos za mwili wake
 
STEVEN GERRARD (IBIZA)
Kwa upande wa kiungo nguli wa Liverpool  Steven Gerrard naye alikuwa katika pwani ya Ibiza akiwa na mkewe Alex.
Gerrards alielekea huko kwa ajili ya kuogelea katika pwani hiyo ya bahari ya Mediterranean ambapo maji yalikuwa yabaridi sana.
Nahodha huyo wa Liverpool pia alikutana na nyota mwenzake wa zamani ndani ya Anfield Jamie Carragher, ambaye aliastaafu rasmi mwishoni mwa msimu.
Gerrard hajaonekana dimbani tangu mchezo wa Merseyside derby mwanzoni mwa mwezi May, baada ya klabu yake kuthibitisha kuwa kiungo atakosekana mpaka kumalizika kwa msimu kufuatia upasuaji ya bega.
Kiungo huyo anatarajiwa kuwa sawasawa katika kipindi cha kuanza kwa msimu.
Splash: Steven and Alex Gerrard went for a dip in the sea during their holiday in Ibiza
Steven na Alex Gerrard wakiingia zaidi katika maji wakati wa mapumziko yao huko Ibiza

Never walk alone: Former team-mates Gerrard and Jamie Carragher enjoyed the sun at an Ibiza beach last week
Never walk alone: Gerrard na Jamie Carragher

DAVID BECKHAM (CHINA)
David Beckham amesafiri kuelekea China , ambako amekubali kufanya kazi ya ubalozi wa soka la nchi hiyo duniani.
Nhodha huyo wa zamani wa England alipewa kazi hiyo mwezi machi kwa lengo kuamsha upya soka la China.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 alitangaza kuacha soka mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kuitumikia Paris Saint-Germain nusu msimu.
Beckham alivitumikia vilabu mbalimbali vikubwa duniani ikiwemo Manchester United, Real Madrid  AC Milan.
On tour: David Beckham is on a week-long trip to China, where he is a global football ambassador
David Beckham akiwa safarini akielekea China, ambako atafanya kazi ya ubalozi wa soka

 Ambassador: Beckham talks to media after arriving in Beijing
Blozi Beckham akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili Beijing

Good cause: Beckham visits Soong Ching Ling's Former Residence to donate a car to his foundation
Balozi Beckham akitembelea Soong Ching Ling

KYLE WALKER na JONNY EVANS (BARBADOS)
Msimu umemalizika lakini hiyo si kwamba imemaliza kukutana kwa Manchester United dhidi ya Tottenham nje ya Old Trafford au  White Hart Lane, ilikuwa ni makutano ya kirafiki na maelewano baina ya Kyle Walker na Jonny Evans katika pwani ya Barbados.

Mlinzi wa kimataifa wa Ireland ya kaskazini Evans akiwa na mpenzi wake mtangazji wa MUTV Helen McConnell, ambao waliona kiangazi hii.
Fancy seeing you here: United defender Jonny Evans ran into Tottenham's Kyle Walker in Barbados
Mlinzi wa United Jonny Evans akimfuata Kyle Walker wa Tottenham pwani ya Barbados walipokutana.

RAISI JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA KLABU YA SUNDERLAND YA UINGEREZA






TAIFA STARS NA IVORY COAST WAINGIZA MILLIONI 500 HUKU BAADA YA KUIKOSA SAFARI YA BRAZIL 2014 - TAIFA STARS SASA KUINGIA KAMBINI JULAI 4 - SAMATTA NA ULIMWENGU WATEMWA

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.

Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.

Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

Sunday, June 16, 2013

MTANANGE WA STARZ NA TEMBO KATIKA PICHA


 Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars'
Kikosi cha Ivory Coast.
 Waamuzi wa mechi ya Stars na Ivory Coast wakiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili. 
Benchi la ufundi la timu ya Taifa Stars. 
 Benchi la ufundi la timu ya Ivory Coast.
 Thomas Ulimwengu akimtoka mchezaji wa Ivory Coast, Bamba Souleman
 Ni hatari.
 Heka heka.
Gooooooooo. 

 Thomas Ulimwengu akishangilia bao la pili la Stars.
Mashabiki wakishangilia.
Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Ivory Coast. Stars ilifungwa 4-2. 
 Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen akilalamikia penalti iliyotolewa na mwamuzi, Mehdi Abid.  
 Beki wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Ivory Coast, Aurier Alain katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia uliuofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa Ivory Coast wakisalimia na wenzao.
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Amri Kihemba akiwatoka mabeki wa timu ya Ivory Coast,  katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Ivory Coast ilishinda 4-2. 
Mshambuliaji wa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka, Bamba Souleman.