KIUNGO Jesus Navas amesema anafurahia kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini.
Navas anatua Etihad kwa dau la Pauni
Milioni 23 kutoka Sevilla huku kocha wa Malaga, Pellegrini anajiandaa
kuthibitishwa kurithi mikoba ya Roberto Mancini.
Winga huyo wa kulia, ambaye amekuwa
akichezea tangu anaibuka hadi sasa, anaamini uhamisho huo utakuwa wa
mafanikio kwa wote, klabu na mchezaji.

Jesus Navas (kushoto) anafurahia kujiunga na Manchester City kutoka Sevilla

Kocha mpya: Manuel Pellegrini anajiandaa kuthibitishwa kocha mpya Etihad baada ya kufukuzwa kwa Roberto Mancini
"Nina furaha kujiunga na Manchester City. Ni nafasi nzuri kwangu na ninafikiri pande zote zina furaha. Niliamua kujiunga na City miezi minne iliyopita. Bado sijazungumza na Manuel Pellegrini, lakini ni kocha ninayemfahamu,".
Navas, aliichezea Hispania katika
Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010, amesema hafahamu kama nyota
mwenzake wa La Liga, Isco, anayechezea timu ya Pellegrini, Malaga naye
anakuja City.

Nyota wa taifa: Navas ameitwa kwenye kikosi cha Kombe la Mabara cha Hispania
"Sijui kama Isco atakuja pia. Tutaona.
Ligi Kuu ni ya kasi sana na ninavutiwa nayo, kwa sababu Manchester City
wametengeneza timu nzuri pamoja. Naondoka Sevilla,
ambayo ni sehemu nzuri na ninakwenda katika klabu kubwa England. Bado
siwezi kuzungumza Kiingereza vizuri. Nitajifunza sasa.


Wengine wanaokuja? Thiago Alcantara wa Barca (kushoto) na kiungo wa Malaga, Isco pia wanatakiwa Man City
Isco, pamoja na nyota wa Shakhtar
Donetsk, Fernandinho, kiungo wa Barcelona, Thiago Alcantara, ni baadhi
ya wachezaji wa mwanzoni ambao Pellegrini amewatambulisha wakati City
inapigania saini zao hivi sasa kujenga kikosi cha kurejesha ubingwa wa
Ligi Kuu England, walioupoteza kwa mahasimu wao, Manchester United.
Navas ameichezea mechi 23 nchi yake na
atakuwamo katika kikosi mcha Vincente Del Bosque kitakachoshiriki Kombe
la Mabara baadaye mwezi huu.
No comments:
Post a Comment