Deni
la malimbikizo ya makazi ya waamuzi katika hoteli ya SAFINA
waliochezesha michuano ya Chalenji mwaka 2011 limepelekea hii leo basi
dogo la shirikisho la soka nchini TFF walilopewa na NMB kufungwa
mnyororo ndani viunga vya uwanja wa kumbukumbu ya Karume, kufuatia deni
hilo kufikia zaidi ya shilingi milioni 51. Pichani juu linaonekana basi
dogo aina ya Coaster la udhamini wa NMB likiwa tayari kukokotwa na
Breakdown ya kampuni ya Flamingo Auction Mart kufuatia amri ya mahakama
ya Kivukoni Kinondoni kutolewa kukamtwa kwa mabari mawili likiwemo moja
kubwa lililotolewa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro. Awali deni hilo
lilikuwa ni shilingi milioni 21 lakini kuchelewa kulipwa kwa deni hilo
kumepelekea deni hilo kufikia shilingi milioni 51. Hata hivyo baada ya
mazungumzo marefu baina ya katibu wa TFF Angetile Oseah na maafisa wa
kampuni ya Flamingo hatimaye basi hilo lilinusurika kuondolewa kwa kile
kilichoelezwa kuwa TFF ilipunguza deni hilo kwa pesa taslimu. |
No comments:
Post a Comment