Meireles alionyesha kifua chake kilichojaa tattoo akiwa na mkewe ufukweli huko Miami, Gerrards ufukweni Ibiza na Beckham arejea kazini Uchina
Baada ya msimu mgumu wa soka kote duniani, wachezaji wa soka duniani wamekuwa katika msimu wa mapumziko ya kiangazi.
Rockersports kupitia mtandao wa Sportsmail
inaendelea kukupatia hatua za mapumziko ya wachezaji hao kutoka Las
Vegas, mpaka Dubai, Ibiza na kurejea Las Vegas kila siku fuatilia.
RAUL MEIRELES (MIAMI)
Kiungo
wa kireno Meireles ameonekana akivinjari huku akiuanika mwili wake
uliojaa tatoo juani katika pwani ya Miami akiwa na mpenzi wake Ivone
ambaye naye mwili wake umejaa mitatoo.
Meireles
alielekea
England mwaka 2010 alipojiunga na Liverpool akitokea Porto ya Ureno.
Baadaye alijiunga na Chelsea na kujiunga na meneja wake wa zamani
alipokuwa Porto Andre Villas-Boas.
Kiungo
huyo mwenye umri wa miaka 30 baadaye akajiunga na Fenerbahce ya Uturuki
msimu uliopita kwa uhamisho wa pauni milioni £8 ambapo aliungana na
nyota mwenzake katika klabu ya Liverpool
Dirk Kuyt.

Kiungo mreno Raul Meireles akiwa na mkewe Ivone ndani ya ufukwe ya Miami

Ivone Meireles akionyesha tattoos za mwili wake
STEVEN GERRARD (IBIZA)
Kwa upande wa kiungo nguli wa Liverpool
Steven Gerrard naye alikuwa katika pwani ya Ibiza akiwa na mkewe Alex.
Gerrards
alielekea huko kwa ajili ya kuogelea katika pwani hiyo ya bahari ya Mediterranean ambapo maji yalikuwa yabaridi sana.
Nahodha
huyo wa Liverpool pia alikutana na nyota mwenzake wa zamani ndani ya
Anfield Jamie Carragher, ambaye aliastaafu rasmi mwishoni mwa msimu.
Gerrard
hajaonekana dimbani tangu mchezo wa Merseyside derby mwanzoni mwa mwezi
May, baada ya klabu yake kuthibitisha kuwa kiungo atakosekana mpaka
kumalizika kwa msimu kufuatia upasuaji ya bega.
Kiungo huyo anatarajiwa kuwa sawasawa katika kipindi cha kuanza kwa msimu.

Steven na Alex Gerrard wakiingia zaidi katika maji wakati wa mapumziko yao huko Ibiza

Never walk alone: Gerrard na Jamie Carragher
DAVID BECKHAM (CHINA)
David Beckham amesafiri kuelekea China , ambako amekubali kufanya kazi ya ubalozi wa soka la nchi hiyo duniani.
Nhodha huyo wa zamani wa England alipewa kazi hiyo mwezi machi kwa lengo kuamsha upya soka la China.
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 38 alitangaza kuacha soka mara baada ya
kumalizika kwa msimu uliopita baada ya kuitumikia Paris Saint-Germain
nusu msimu.
Beckham alivitumikia vilabu mbalimbali vikubwa duniani ikiwemo Manchester United, Real Madrid AC Milan.

David Beckham akiwa safarini akielekea China, ambako atafanya kazi ya ubalozi wa soka

Blozi Beckham akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili Beijing

Balozi Beckham akitembelea Soong Ching Ling
KYLE WALKER na JONNY EVANS (BARBADOS)
Msimu
umemalizika lakini hiyo si kwamba imemaliza kukutana kwa Manchester
United dhidi ya Tottenham nje ya Old Trafford au White Hart Lane,
ilikuwa ni makutano ya kirafiki na maelewano baina ya Kyle Walker na
Jonny
Evans katika pwani ya Barbados.
Mlinzi
wa kimataifa wa Ireland ya kaskazini Evans akiwa na mpenzi wake
mtangazji wa MUTV Helen McConnell, ambao waliona kiangazi hii.

Mlinzi wa United Jonny Evans akimfuata Kyle Walker wa Tottenham pwani ya Barbados walipokutana.
No comments:
Post a Comment