KOCHA
Arsene Wenger amesema hana mzaha na hatabadlisha mawazo katika suala la
kumsajili mshambuliaji 'aliyetikiswa' Manchester United, Wayne Rooney.
Nyota
huyo wa England, ambaye alifunga bao zuri katika sare ya 2-2 dhidi ya
Brazil usiku wa jana, ameonyesha nia yake ya kuondoka Manchester United
msimu huu.
Mwezi uliopita,Sportsmail ililipua habari kwamba Arsenal wako tayari na wanajiamini watavunja rekodi yao ya dau la usajili kumsajili Rooney.

Mtafutwaji: Wayne Rooney inaaminika anataka kuondoka Manchester United
Na Wenger ametilia msistizo kauli yake, akisema yuko tayari kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
"Rooney anaweza kuwa mchezaji anayemvutia kila mtu duniani, nani anayeweza kumpiga chini yeye?" Wenger aliiambia Al Jazeera.
Wenger
pia anataka kumrejesha Nahodha wake wa zamani, Cesc Fabregas Emirates
na anaamini kiungo huyo anaumizwa na kukosa namba katika kikosi cha
kwanza cha Barcelona.
Katika
Mkataba wake wakati anaondoka Emirates kwenda Nou Camp mwaka 2011,
ilikubaliwa Arsenal iwe klabu ya kwanza kupewa nafasi ya kumsajili
Mspanyola huyo kwa dau la Pauni Milioni 20, lakini kiwango kinachotakiwa
sasa ni Pauni Milioni 25 kama ada ya uhamisho wake.

Cesc Fabregas aliondoka Arsenal kwenda Barcelona mwaka 2011
No comments:
Post a Comment