Tuesday, June 4, 2013

MOURINHO ANAWATAKA HAWA

KOCHA Jose Mourinho amewalenga wachezaji watano kuwasajili baada ya kurejea Chelsea kwa mara ya pili.
Wachezaji wa mwanzoni anaowataka wanafahamika ni washambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic, Manchester City, Edin Dzeko, sentahafu wa Porto, Eliaquim Mangala, Daniele De Rossi wa Roma na kiungo Mbrazil, Fernandinho wa Shakhtar Donetsk.
Mourinho pia ameweka wazi kumrejesha to Romelu Lukaku, baada ya kufanya vizuri msimu huu akiwa na West Brom ambako amefunga mabao 17, kwamba hataki atolewe kwa mkopo tena. 
The second coming: Jose Mourinho signed a four-year deal to seal a return to Chelsea, where he left in 2007
Jose Mourinho amesaini Mkataba wa miaka minne kurejea Chelsea, alipoondoka mwaka 2007
New faces: Mourinho doesn't want Romelu Lukaku back out on loan while Daniele De Rossi (below) is a target
Sura mpya: Mourinho hataki Romelu Lukaku atolewe tena kwa mkopo waakti anamtaka na Daniele De Rossi (chini)
Daniele De Rossi
Kevin de Bruyne, ambaye ameomba kuuzwa moja kwa moja Borussia Dortmund baada ya kucheza kwa mkopo Werder Bremen, atakutana na kocha huyo mpya kabla ya kufikiwa uamuzi juu ya mustakabali wake.
Lakini Mourinho amesistiza hatafanya mabadiliko makubwa msimu huu, akisema: "Tunatakiwa kuimarisha timu, na ninaposema naimarisha timu, watu tayari wanafikia mamilioni mangapi Chelsea watatumia.
"Lakini ninaposema naimarisha timu nasema kuimarisha kwa kazi. Kazi yangu lazima iimarishe wachezaji na kuimarisha timu. Ikiwa sitafanya hivyo sitakuwa na furaha binafsi.  
"Ikiwa baada ya hapo tutaimarisha timu kwa kununua wachezaji wachezaji wachache, itakuwa nzuri. Nataka kuanzia chini sifuri, nahitaji kufanya kazi ngumu tena na ujenga timu tofauti na ile niliyojenga wakati ule. Nataka kusahau kwamba nilikuwa bingwa hapa na ninataka niwe hamasa hiyo binafsi kama nipo hapa kwa mara ya kwanza,"alisema. 
Most wanted: Fiorentina striker Stevan Jovetic
Anayetakiwa zaidi: Mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic
Target: Porto's French defender Eliaquim Mangala (right)
Beki wa Porto, Mfaransa Eliaquim Mangala (kushoto) anatakiwa pia
Midfield general: Fernandinho played against Chelsea last season for Shakhtar
Kiungo Fernandinho alicheza dhidi ya Chelsea msimu uliopita akiwa Shakhtar

No comments:

Post a Comment