Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea kwa
mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa
kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangweha, aliyefariki huko Afrika
Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa katika shughuli za muziki, Jumanne tarehe 28 Mei, 2013.
Kifo cha Albert Mangweha ni pigo kubwa kwa fani ya muziki hapa
nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika fani hiyo
ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji ya “Free Style”
alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana ndani na nje ya nchi.
Albert Mangweha atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa muziki kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote na kuwaomba wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangweha
mahala pema peponi.”
Imetolewa na
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo
Dkt Fenella Mukangara
|
No comments:
Post a Comment