SIMBA
SC imekamilisha usajili wa kikosi cha msimu ujao kwa asilimia 80 na
ndani yake itakuwa na wachezaji wanne wa kigeni, akiwemo mshambuliaji
Moses Oloya kutoka Uganda.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia MPIRA MAENDELEO leo kwamba wamekamilisha mazungumzo na kufikia makubaliano na
Oloya, na sasa kuna kitu kimoja wanasubiri kabla ya kusaini naye
mkataba.
“Timu
ya taifa ya Uganda inakwenda Libya kucheza mechi za kufuzu za Kombe la
Dunia. Akimaliza anakwenda kwenye klabu yake kuchukua barua ya
kututhibitishia hana mkataba, ndipo tutampa chake naye asaini,”alisema HANS POP ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuhakikisha CHAMA LA WANA linatisha msimu ujao kuanzia kwenye michuano ya KAGAME.
Friday, May 31, 2013
CHAMA LA WANA MDOGO MDOGO LINAJIJENGA USAJILI ASILIMIA KUBWA OYAA OYAA TUNAISUBIRI KAGAME
Thursday, May 30, 2013
LIVERPOOL YABOMOKA JAMANI
MSHAMBULIAJI
Luis Suarez amezua hofu juu ya mustakabli wake katika klabu ya
Liverpool baada ya kusema itamuwia vigumu kukataa ofa ya Real Madrid.
Suarez,
anayetumikia kifungo cha adhabu ya mechi 10 kwa kumng'ata beki wa
Chelsea, Branislav Ivanovic, amesema katika mahojiano na kituo cha Redio
cha Uruguay analazimika kuondoka kutokana na jinsi anavyoshambuliwa na
vyombo vya habari England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema: "Liverpool wanataka nibaki, lakini ngumu kuwakatalia Real Madrid.

Mtikisiko: Suarez amesema itakuwa ngumu kuikatalia Real Madrid
"Nina familia ambayo pia inaathiriwa na hali hii na imevuka kiwango.
"Sijiandai
kupambana na Waandishi wa Habari wa England. Nimepambana sana tangu
nikiwa mdogo kufika hapa nilipo, kuwaacha waandishi fulani wanitendee
ubaya.
"Hawanihukumu
kama mimi ni mchezaji, bali mtazamo wangu. Wananizungumzia kana kwamba
wanafahamu maisha yangu yote vizuri. Nina mke na mtoto wa kike na siko
tayari kuendelea kupambana na vyombo vya habari vya England,"alisema.
Liverpool imesistiza Suarez hauzwi na kwamba kwa kuwa alisani mkataba mpya wa miaka minne msimu uliopita, wanatarajia atabaki.


Suarez kwa sasa yupo na timu yake ya taifa, Uruguay

Kocha
Brendan Rodgers hana presha ya kumuuza mchezaji huyo, lakini Madrid
wanaandaa Pauni Milioni 25 na wachezaji wawili, washambuliaji chipukizi
Alvaro Morata na Jese Rodriguez.
Liverpool
pia inakabiliwa na mtihani wa kumzuia kipa Pepe Reina anayetakiwa
Barcelona ambaye amesema wazi itakuwa vigumu kukataa ofa ya vigogo wa
Catalan.
"Ni
vigumu kuwakatalia Barca, pamoja na kwamba sina uhakika kama
wananihitaji kwa dhati,' alisema mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka
30.

Aspas amefanya vizuri katika msimu wake huu wa kwanza La Liga
Lakini
Liverpool imeimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kukubali kumsajili
kwa Pauni Milioni 6, mshambuliaji wa Celta Vigo, Iago Aspas, mwenye umri
wa miaka 25, ambaye anaweza kucheza katikati au pembeni.
Huku
Celta Vigo ikikabiliwa na hatari ya kushuka Daraja dau hilo ni punguzo
kutoka Pauni Milioni 8 na Aspas atafanyiwa vipimo vya afya wiki ijayo.
BALOZI WA TANZANIA ETHIOPIA AWAPA CHANGAMOTO STARS ADDIS
Na Boniface Wambura, Addis Ababa
BALOZI
wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa
Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la
Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Ametoa
changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29
mwaka huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
imepiga kambi nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis
Ababa.
“Watanzania
tunafurahi kutokana na uwezo mnaouonyesha, hasa baada ya kuifunga
Morocco mabao 3-1. Kama mliwafunga nyumbani hata kwao mnaweza kuwafunga.
Tunataka kuwaona Maracana (Brazil) mwakani, mimi tayari ninayo tiketi
mtanikuta kule,” amesema Balozi Biswaro ambaye enzi zake aliwahi
kuichezea timu ya Yanga.
Taifa
Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka
kambi katika hoteli ya Hilton ambapo Jumapili (Juni 2 mwaka huu)
itacheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile) kwenye Uwanja wa
Addis Ababa.
Balozi
Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya
mechi dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi
Ethiopia kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri.
Kocha
Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na
kitaimarika zaidi baada ya wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
kujiunga nacho Juni 3 mwaka huu jijini Marrakech kwa ajili ya mechi
dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu.
Wachezaji
walioko katika kikosi cha Stars jijini Addis Ababa ni Juma Kaseja,
Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin
Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo,
Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva,
John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haroun
Chanongo na Zahoro Pazi.
Wednesday, May 29, 2013
UNYAMA UNAYAMANI KAMA KAWA CHAMA LA WANA LIMEANZA KUPIGA TIZI KINES TAYARI KURUDISHA HESHIMA MJINI
![]() |
Kocha mpya wa Simba SC, Alah Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden' akitoa maelekezo kwa wachezaji |
![]() |
King Kibaden kazini |
![]() |
Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelo 'Julio' akimhoji Mnigeria Izdore kabla ya kuanza mazoezi |
![]() |
Cheki vipaji Simba SC... |
![]() |
Issa Rashid 'Baba Ubaya' kushoto akimgeuza mtu... |
![]() |
Izdore akikaba ng'ado kwa ng'ado... |
![]() |
Jamhuri akizungumza na Nassor Masoud 'Chollo(KWA HISANI YA BIN ZUBEIRY) |
WATAELEWA TU NINI SIMBA INAMAANISHA Moses Oloya KAMA KUNA MASWALI MAJIBU ANAYO HANS POP
SIMBA
imeonyesha kweli imepania kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada
ya kumnasa kiungo mshambuliaji nyota kutoka Uganda, Moses Oloya.
Simba
imelazimika kujipinda na ‘kuvunja benki’ kwa kutoa zaidi ya Sh milioni 40 ili
kumsajili Oloya ikiwa ni pamoja na kufikia makubaliano na wakala wake aliyejulikana
kama DM Management.
Oloya
ambaye amekuwa akiwagawa mashabiki wa soka Uganda, kwamba yeye na Okwi nani ni
zaidi, amekubali kumwaga wino na kuichezea Simba msimu ujao.
Kila kitu
kati ya Oloya na Simba kimemalizika na mchezaji huyo amekubali kuondoka Xuan
Than Saigon inayoshiriki Ligi Kuu ya Vietnam na kujiunga na Simba.
Simba
imekuwa ikifanya siri kubwa kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo wakiwahofia
watani wao Yanga wanaweza kuvuruga mambo na kumsajili.
“Yanga
ndiyo imekuwa hofu kubwa, maana wakisikia Simba wanamhitaji mchezaji na wenyewe
wanamuona anafaa. Hilo ndiyo limekuwa tatizo kwetu.
“Lakini
Oloya amekubali kusaini, mkataba wake utatumwa huko kwa kuwa Uganda The Cranes
itakuwa huko kucheza mechi ya kirafiki Jumamosi hii.
“Kila kitu
kitamalizikia Libya, labda kama kuna mabadiliko lakini kila kitu kimefikiwa
makubaliano,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Oloya
ambaye ana miaka 20 tu, alijiunga na Xuan Than Saigon, Januari Mosi, 2011 na
amefanikiwa kufunga katika mechi kadhaa za kirafiki ingawa anaonekana kuwa
mzuri katika kupiga mabao.
Urefu wake
ni futi 1.80, ana kasi inayolingana na ile ya Okwi, anapiga mashuti miguu yote,
si mzuri sana wa mipira ya vichwa, ana uwezo wa kupiga mipira iliyokufa.
Ndiye
anaaminika kuwa staa mpya wa Uganda ambayo tayari kaichezea mechi 14, mashabiki
wengi wamekuwa wakiamini ni mkali kuliko Okwi.
Tayari
Oloya amejiunga na kikosi cha Uganda nchini Libya, tayari kwa ajili ya mechi
hiyo ya kirafiki dhidi ya wenyeji.
Monday, May 27, 2013
REAL MADRID YAMPA ZIDANE KAZI YA KUHAKIKISHA BALE ANATUA SANTIAGO
MMOJA wa wachezaji nyota historia ya Real Madrid, Zinedine Zidane amepewa jukumua la kuhakikisha nyota wa Tottenham, Gareth Bale anatua Bernabeu kwa dau la Pauni Milioni 65.
Gazeti la Hispania, Marca limeripoti kwamba Galactico
huyo wa zamani, Zidane ni mshauri mkuu katika mpango wa usajili huo na
anajaribu kumshawishi Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwamba
saini ya Bale ni kitu pekee muhimu.


Kipaumbele namba 1: Gwiji wa Real na
Ufaransa, Zinedine Zidane (kushoto) na mchezaji anayewaniwa na klabu
nyingi Ulaya, Gareth Bale (kulia)

Mpiga debe: Zinedine Zidane amesema Gareth Bale ni zaidi ya bora kiasi cha kutosha kucheza Real Madrid
"Kitu ambacho kimenivutia kwa ujumla ni kwamba ana muendelezo wa ubora. siyo wa mechi moja au mbili.Zidane
ambaye anamzimikia kwa muda mrefu nyota huyo wa Wales, amesema:
"Nimekuwa nikiitazama Tottenham kwa sababu Gareth Bale amekuwa akicheza
huko. Mbali na Ronaldo na Messi, ndiye mchezaji ambaye amekuwa
akinivutia zaidi duniani. Ni wa uhakika,".
"Anaendeleza kufunga mabao mazuri na muhimu. Ni mwepsi sana, mwenye kipaji na anayevutia.
"Ndiyo, wachezaji wenye kipaji kama yeye
wanaweza kuja Real Madrid. Ni mzuri kiasi cha kutoha kwa Real Madrid?
Ndiyo. Ni zaidi ya mzuri kiasi cha kutosha kucheza Real Madrid.’
Zidane alikuwa mchezaji mtu muhimu
katika biashara ya usajili Madrid tangu astaafu mwaka 2006. Alichangia
mno kutua kwa Raphael Varane Bernabeu na ana matumaini ya kumleta Bale
katika njia ile ile.

Kivutio: Bale akiichezea Spurs. Amemvutia Zidane msimu huu


Baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, Bale ndiye mchezaji anayemvutia zaidi Zidane
CHRIS SMALLING ANAPONYA KIDONDA CHA UPASUAJI KWA MSAADA WA MPENZI WAKE SAM COOKE
![]() |
Hard work, this rehab lark: Smalling's making sure he keeps his feet up after a long season. |
Mlinzi
wa kati wa Manchester United Chris Smalling amekuwa akiendelea kuponya
kidonda chake cha baaba ya upasuaji wa mguu wa mguu wake wa kulia akiwa
katika pwani ya Barbados fakipunga upepo wa pwani wenye joto akiwa na
mpenzzi wake Sam Cooke.
Akiwa
ameongozana na mpenzi wake huyo katika mapumziko ya kumaliza wiki
amekuwa akijitahidi kufanya mazoezi madogo madogo kulinda uzito wake na
kuimarisha mguu huo.
Mlinzi huyo anatarajiwa kuwa sawa katika kipindi cha matayarisho ya kuanza msimu mpya.
Meneja
mpya wa Manchester United David Moyes atakuwa na kazi ya kujenga timu
mpya itakayokuwa na vipaji vichanga kama ilivyo kwa wachezaji kama
Smalling,
Phil Jones na Tom Cleverley.

Helping hand: Chris Smalling's girlfriend Sam Cooke helps him keep his weight off of his injury
Smalling
mwenye umri wa miaka 23, pia atakosekana katika kikosi cha timu ya
taifa ya England kitakachokuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi
ya Jamhuri ya Ireland lakini pia katika safari ya kuelekea nchini Brazil
kufuatia kuaendelea kuuguza mguu wake.
Bosi wa England Roy Hodgoson amekaririwa kisema
‘Sasa ndio fursa kwakuwa Smalling na Jones kama ilivyo kwa wastaafu Rio Ferdinand na John Terry waliostaafu soka la kimataifa.
'Wamepata
nafasi, jambo ambalo ni muhimu. Rio na John wamefanya kazi nzuri sana
kwa kipindi chote. Sasa wameondoka ni jukumu kwa vijana hawa kutazama
mbele.

Chris
Smalling akimtazama kwa nyuma mpenzi wake Sam Cooke akitembea kutafuta
viburudisho katika pwani ya Barbados Jumapili ya jana.





Smalling na mpenzi wake Sam wakiwa majini.




The high life: Martin Skrtel and wife Barbora take it easy on Miami beach

Going for a stroll: Mind that foot though, Martin
John Mikel Obi sasa kuichezea Nigeria michuano ya mabara, Torres aitwa timu ya taifa ya Hispania, Lazio yatwaa taji la Copa Italia na Cristal Palace yapanda daraja.
Kiungo wa Chelsea
John Mikel Obi amethibitisha kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kuelekea
katika michezo ya kufuzu kombe la dunia na kichuano ya kombe la shirikisho nchini Brazil.
Mikel alikuwa
katika mashaka makubwa kufuatia kuwa katika majukumu na klabu yake lakini pia
kutokana na tatizo la visa.
Shirikisho la
soka la nchini Nigeria (NFF) limetanabaisha kuwa kiungo huyo mwenye umri wa
miaka 26 hatakuwepo katika mchezo wa kimataifa wa kirafikia dhidi ya Mexico May
31.
Hata hivyo
shirikisho hilo limethibitisha kuwa atapatikana katika michezo miwili dhidi ya Kenya
na Namibia, pamoja na michezo ya michuano ya shirikisho yaani Confederations Cup.
Kueleka katika
michezo yao ya hivi karibu mwezi wa juni mabingwa hao wa soka barani Afrika
watakuwa wakiwakosa wachezaji wao wakali wakiwemo majeruhi Victor Moses, Kalu
Uche na Gabriel Rueben.
Watamkosa pia
mfungaji bora wa fainali za mataifa ya Afrika Emmanuel Emenike, ambaye
anasumbuliwa na mguu.
Super Eagles
wako sawa kwa alama na Malawi katika kundia F la kuwania kufuzu kombe la dunia
wakiwa wote wana alama tano wakati ambapo kiongozi wa kundi akitarajiwa kusonga
mbele katika changamoto nyingine ya kusaka nafasi ya kufuzu.
Baada ya kufunga bao europa league Fernando Torres aitwa kikosini Hispania kucheza kombe la mabara
Mshambuliaji
aliyekuwa hapewi nafasi ya kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa kutoka na
kiwango chake kutoridhisha Fernando Torres ametajwa na Hispania kujiunga katika
kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la
shirikisho la mabara.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka , 29, ambaye akiwa na klabu yake alifanikiwa kutwa
taji la Europa League msimu huu hivi karibuni alishindwa kumshawishi kocha Vicente
del Bosque katika kikosi chake.
Wengine wanane
wanaocheza cheza soka nchini England wameitwa ambapo baadaye kikosi hicho
kitapunguzwa kutoka jumla ya wachezaji 26 na kusaliwa na wachezaji 23 kabla ya
kuaanza kwa michuano hiyo nchini Brazil june 15.
Mlinzi wa Barcelona
Carles Puyol na mshambuliaji wa Sevilla Alvaro
Negredo wameachwa na kocha huyo.
Mlinda mlango
wa Real Madrid na nahodha wa Hispania aliyevunjika kidole mwezi Januari Iker
Casillas wamerudishwa huku kiungo Javi Martinez aliye katika kiwango safi akiwa
na Bayern Munich ambao wametwaa taji la Champions League wote wameitwa.
Torres alikuwa
na msimu mzuri akiwa na Chelsea akifunga jumla ya magoli 22 baada ya kucheza
michezo 64 ikiwa ni pamoja na kufunga goli la kwanza katika mchezo wa ushindi
wa mabao 2-1 wa fainali ya Europa dhidi ya Benfica.
Goalkeepers:
Iker Casillas (Real Madrid), Jose Reina (Liverpool), Victor Valdes (Barcelona).
Defenders:
Jordi Alba (Barcelona), Raul Albiol (Real Madrid), Alvaro Arbeloa (Real
Madrid), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Nacho Monreal (Arsenal), Gerard Pique
(Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid).
Midfielders:
Xabi Alonso (Real Madrid), Benat Etxebarria (Real Betis), Sergio Busquets
(Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Cesc Fabregas (Barcelona), Javi Garcia
(Manchester City), Andres Iniesta (Barcelona), Javi Martinez (Bayern Munich),
Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla), Pedro (Barcelona), David Silva
(Manchester City) Xavi (Barcelona).
Forwards:
Fernando Torres (Chelsea), Roberto Soldado (Valencia), David Villa (Barcelona).
Lazio yatwaa Coppa Italia baada ya kuwafunga Roma katika fainali
Lazio imeshinda
taji la Coppa Italia kwa mara ya sita baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
wapinzani wao wakubwa Roma mchezo uliopigwa Stadio Olimpico.
Senad Lulic alifunga
bao pekee la ushindi kwa mabingwa hao kufuatia mlinda mlango wa Roma Bogdan
Lobont kushindwa kuifuata krosi ya Antonio Candreva.
Nafasi kubwa
ya Roma kusawazisha ilikuwa pale mpira wa adhabu ya moja kwa moja uliopigwa na
mkongwe Francesco Totti kugonga mtamba wa panya.
Ushindi wa Victory
Lazio, ambao walimaliza msimu katika nafasi ya saba katika ligi kuu ya Italia Serie
A, unamaanisha kuwa watakuwa wamefuzu moja kwa moja kucheza Europa League hatua
ya makundi.
Lazio imeshinda
mara nne katika mara tano walizokutana na wapinzani wao wakubwa hao huku
matokeo mengine yakiwa ni sare ya 1-1 mwezi April.
CRISTAL
PALACE YAPANDA DARAJA
Mkongwe
Kevin Phillips hii leo ameifungia goli muhimu kwa Crystal Palace
iliyokuwa bora na iliyostahili kuichapa Watford katika mchezo wa fainali
wa Championship play-off uliopigwa katika dimba la Wembley.
Mkongwe
huyo mwenye umri wa miaka 39 alifunga goli hilo kwa mkwaju wa penati
katika dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza na kumaliza kiu ya
kusubiri kwa miaka nane kupanda daraja na kucheza ligi kuu ya soka
nchini England Premier League.
Ilkuwa
ni penati nzuri iliyotokana na mlinzi Marco
Cassetti wa Watford kumfanyia madhambi mshambuliaji mtarajiwa wa
Manchester United Wilfried Zaha, ambaye amekuwa katika kikosi cha Palace
tangu akiwa na umri wa miaka tisa na akicheza mchezo wa fainali kabla
ya kuelekea kwa Manchester United wakati wa kipindi cha uhamisho cha
majira ya kiangazi.
Ushindi huo unawafanya Crystal Palace kuungana sasa na kikosi cha meneja Ian Holloway cha Blackpool kucheza ligi hiyo.
WAO KELELE SISI KIMYA KIMYA TUTAKUTANA SUDAN
kitasa kipya mitaa ya unyama unyamani aka msimbazi
SIMBA
SC imeendelea na harakati za ujenzi wa kikosi kipya hatari cha msimu
ujao, baada ya saa mbili zilizopita kukamilisha usajil iwa beki wa kati
wa kimataifa wa Uganda, Samuel Ssenkoomi anayechezea timu ya Mamlaka ya
Mapato Uganda (URA).
Habari za ndani ambazo MPIRA MAENDELEO imezipata kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Ssenkoomi amesaini mkataba wa miaka miwili kuchezea Wekundu hao wa Msimbazi.
Huyo anakuwa Mganda wa tatu katika kikosi cha Simba SC baada ya kipa, Abbel Dhaira na kiungo Mussa Mudde na inawezekana hadi wiki ijayo, Wekundu hao wa Msimbazi wakatimiza idadi ya wachezaji wanne kutoka nchi hiyo, kwani hivi sasa wako mbioni kuinasa saini ya mshambuliaji hatari mno wa The Cranes.
Aidha, beki huyo mwenye nguvu na akili za mpira, anakuwa mchezaji wa tano mpya kusajiliwa Simba SC kwa ajili ya msimu ujao, baada ya awali kusajiliwa wachezaji wanne wazawa, kipa Andrew Ntalla kutoka Kagera Sugar, beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar, kiungo Twaha Shekuwe ‘Messi’ kutoka Coastal Union na mshambuliaji Zahor Pazi kutoka Azam FC aliyekuwa anacheza kwa mkopo JKT Ruvu.
Simba SC imepania kuboresha kikosi chake ili kurejesha makali yake msimu ujao, baada ya msimu huu kutoka mikono mitupu, ikivuliwa ubingwa na kukosa hata nafasi ya pili, ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba SC ambayo mzunguko wa kwanza ilikuwa chini ya Mserbia, Milovan Cirkovick na mzunguko wa pili chini ya Mfaransa Patrick Liewig, imemaliza Ligi Kuu katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga mabingwa.
Kocha Mfaransa Patrick Liewig amepewa mishahara yake ya miezi miwili, Sh. Milioni 12 aliyokuwa anadai na tiketi ya kurejea kwao moja kwa moja na Abdallah Athumani Seif, maarufu ‘Kingi Kibadeni’, bila shaka atasaini mkataba wakati wowote kurithi mikoba.
Liewig sasa atakuwa anadai mshahara wa mwezi mmoja, Mei ambao uko ukingoni yeye akiwa tayari Ufaransa.
Simba SC pia imewaongezea mikataba wachezaji wake chipukizi kadhaa iliyowapandisha kutoka kikosi cha pili akiwemo Haruna Chanongo, ambaye alikuwa anapigiwa hesabu na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Simba sasa inaelekeza nguvu zake katika usajili wa mshambuliaji sambamba na kusaini mikataba mipya na Nahodha wake Juma Kaseja pamoja na kiungo Amri Kiemba
Habari za ndani ambazo MPIRA MAENDELEO imezipata kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Ssenkoomi amesaini mkataba wa miaka miwili kuchezea Wekundu hao wa Msimbazi.
Huyo anakuwa Mganda wa tatu katika kikosi cha Simba SC baada ya kipa, Abbel Dhaira na kiungo Mussa Mudde na inawezekana hadi wiki ijayo, Wekundu hao wa Msimbazi wakatimiza idadi ya wachezaji wanne kutoka nchi hiyo, kwani hivi sasa wako mbioni kuinasa saini ya mshambuliaji hatari mno wa The Cranes.
Aidha, beki huyo mwenye nguvu na akili za mpira, anakuwa mchezaji wa tano mpya kusajiliwa Simba SC kwa ajili ya msimu ujao, baada ya awali kusajiliwa wachezaji wanne wazawa, kipa Andrew Ntalla kutoka Kagera Sugar, beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar, kiungo Twaha Shekuwe ‘Messi’ kutoka Coastal Union na mshambuliaji Zahor Pazi kutoka Azam FC aliyekuwa anacheza kwa mkopo JKT Ruvu.
Simba SC imepania kuboresha kikosi chake ili kurejesha makali yake msimu ujao, baada ya msimu huu kutoka mikono mitupu, ikivuliwa ubingwa na kukosa hata nafasi ya pili, ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba SC ambayo mzunguko wa kwanza ilikuwa chini ya Mserbia, Milovan Cirkovick na mzunguko wa pili chini ya Mfaransa Patrick Liewig, imemaliza Ligi Kuu katika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga mabingwa.
Kocha Mfaransa Patrick Liewig amepewa mishahara yake ya miezi miwili, Sh. Milioni 12 aliyokuwa anadai na tiketi ya kurejea kwao moja kwa moja na Abdallah Athumani Seif, maarufu ‘Kingi Kibadeni’, bila shaka atasaini mkataba wakati wowote kurithi mikoba.
Liewig sasa atakuwa anadai mshahara wa mwezi mmoja, Mei ambao uko ukingoni yeye akiwa tayari Ufaransa.
Simba SC pia imewaongezea mikataba wachezaji wake chipukizi kadhaa iliyowapandisha kutoka kikosi cha pili akiwemo Haruna Chanongo, ambaye alikuwa anapigiwa hesabu na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Simba sasa inaelekeza nguvu zake katika usajili wa mshambuliaji sambamba na kusaini mikataba mipya na Nahodha wake Juma Kaseja pamoja na kiungo Amri Kiemba
ANGALIA KUFURU YA USAJILI WA SIMBA ILIVYOKUWA, WATATU KWA MPIGO WALIMWAGA WINO HIVI
![]() |
Baba Ubaya akimwaga wino mbele ya Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'are aka Mzee Kinezi |
kwa hisani ya salehjembe.blogspot.com
UONGOZI wa
Simba umeonyesha umepania kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake msimu
ujao baada ya kusajili wachezaji watatu pamoja katika usiku mmoja.
Simba
imewasajili kipa Andrew Ntalla kutoka Kagera Sugar ambaye atapambana na Juma
Kaseja katika nafasi ya kipa namba moja atakuwepo Simba pamoja na Abel Dhaira
raia wa Uganda.
Imemsajili
beki wa kushoto Issa Rashid maarufu kama Baba Ubaya katika nafasi ya beki wa
kushoto ambayo zaidi alikuwa anategemewa Amir Maftah ambaye yuko kwenye mgogoro
na uongozi wa Simba.
Mchezaji wa
tatu ni Zahoro Pazi, mtoto wa kipa na kocha wa makipa wa zamani wa Simba, Iddi
Pazi ambaye alikuwa anakipiga kwa mkopo JKT Ruvu akitokea Azam FC.
Simba inaonekana
imemchukua Pazi ili kuziba pengo la Mrisho Ngassa aliyekwenda Yanga, Ngassa
alikuwa anacheza zaidi katika winga ya kushoto na mara kadhaa kulia nafasi
ambazo mchezaji huyo mpya anazimudu.
Wachezaji
wote watatu walianguka saini mbele Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph
Itang’are maarufu kama Mzee Kinesi.
![]() |
Messi kutoka Coastal na baba yake mzazi wakiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope. |
Simba
inaendelea kufanya usajili kimya kimya ikilenga kuimarisha kikosi chake kwa
ajili ya msimu ujao ikiwa imelenga kurejesha heshima baada ya kuishia katika nafasi
ya tatu katika msimu uliomalizika Yanga kutwaa ubingwa na Azam FC kushika namba
mbili.
Baba Ubaya
alikuwa ameingia mkataba wa miaka miwili sawa na Pazi wakati Ntalla aliyekuwa
kipa namba moja wa Kagera Sugar iliyoshika nafasi ya nne ikiwa chini ya Abdallah
Kibadeni aliyerejea Simba, yeye amesaini miaka mitatu na wekundu hao wa
Msimbazi.
Tayari
Simba ilifanikiwa kumsajili winga wa Coastal Union Ibrahim Twaha maarufu kama
Messi ambaye mkataba wake ulisainiwa mbele ya baba yake mzazi na Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope.
Simba
imekuwa ikifanya kila namna kuhakikisha usajili wake unakuwa bora ili
kufanikiwa kutwaa tena ubingwa au kuishia katika nafasi ya pili msimu ujao ili
ishiriki michuano ya kimataifa na kurejeshe heshima yake iliyopotea msimu huu.
Bado Simba
inahaha kusajili beki wa kati pamoja na mshambuliaji wa kati, nafasi ambayo
imewasumbua kwa kipindi kirefu kwa karibu msimu wote uliopita, hasa baada ya
Kelvin Yondani kutua Yanga na Mzambia, Felix Sunzu kushindwa kuonyesha cheche.
Subscribe to:
Posts (Atom)