MABINGWA wa Hispania, Barcelona wamekubali kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Neymar kutoka klabu ya Santos.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21,
atasaini mkataba wa miaka mitano, klabu hiyo imesema na mchezaji
mwenyewe amethibitisha atasaini kesho.
Taarifa ya Barcelona imesema: "FC
Barcelona na Santos zimekubaliana kuhusu Neymar da Silva Santos Junior.
Mshambuliaji wa Kibrazil atakuwa mchezaji wa Blaugrana kwa miaka mitano
ijayo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ni miongoni mwa wachezaji
wanaochipukia vizuri duniani.'

Anaondoka: Neymar anaondoka na chini ni ujumbe alioandika kwa ajili ya mashabiki wa FC Santos

Neymar alilazimika kuamua mustakabali
wake, baada ya klabu yake, Santos kusema Ijumaa kwamba wamepokea ofa
mbili kwa ajili ya nyota huyo na Barca ikathibitika kuwa ni moja ya
klabi zilizotoa ofa huku, Real Madrid ikidhaniwa kuwa ni klabu nyingine.
Neymar am,ethibitisha uamuzi wake kwa
kuandika kwenye Instagram: "Nipo hapa na marafiki na familia na
wananisaidia kuandika vitu vichache hapa. Siwezi kusema hadi Jumatatu.
Familia yangu na rafiki zangu tayari wanajua uamuzi wangu.
Jumatatu nitasaini mkataba na Barcelona,".'
Mkataba wake na Santos unatarajiwa
kumalizika msimu ujao na baadhi ya taarifa zinasema kwamba makubaliano
na Barcelona yalifikiwa mwaka mmoja uliopita.
Neymar atawaaga mashabiki wa Santos katika mchezo wa leo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Flamengo.

Anafuata nyayo: Neymar (kulia) amekuwa
akiichezea Santos muda wote na ameichezea timu ya taifa ya Brazil mechi
32. Hapa yupo na Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Mbrazil mwenzake,
Ronaldinho, aliyewahi kung'ara Barcelona
No comments:
Post a Comment