MSHAMBULIAJI Mario Balotelli hastaajabu
Roberto Mancini kufukuzwa Manchester City kwa sababu ya matatizo ya
kocha wake huyo wa zamani na klabu hiyo.
Balotelli, ambaye alisajiliwa na Mancini
City kabla ya kuuzwa AC Milan Januari, amesema Mtaliano mwenzake huyo
ni bonge la kocha.
Mancini alifukuzwa City Jumatatu baada
ya timu kushindwa kufikia malengo yaliyotarajiwa na wamiliki na sasa
nafasi yake inatarajiwa kuzibwa na Manuel Pellegrini wa Malaga.
Angalia video chini

Sacked: But Roberto Mancini, according to Mario Balotelli, is a great manager

Champions: Balotelli (left) and Mancini (centre) at City last May
Alipoulizwa kuhusu kufukuzwa kwa Mancini, Balotelli aliiambia CNN:
"Sishangai kabisa, lakini wakati nilipokuwa naye, alikuwa kocha babu
kubwa na tulikuwa na moja ya timu nzuri kati ya nilizowahi kuchezea,
wachezaji wazuri.
"Sijui kwa nini hakushinda (taji). Lakini dhahiri kulikuwa kuna matatizo ya ndani. Nipo hapa (Milan) hivyo sifahamu,".


Ndondi: Balotelli na Mancini wakikwidana enzi zao Manchester City
No comments:
Post a Comment