KLABU ya Real Madrid iko tayari kuijaribu Tottenham kwa dau la Pauni Milioni 60 kwa ajili ya kumnunua Gareth Bale.
Vigogo hao wa Hispania wamekuwa
wakimtaka Bale kwa zaidi ya mwaka na kocha mpya, Carlo Ancelotti ni
shabiki mkubwa wa winga huyo.
Real wamepania kuibuka msimu ujao, baada ya msimu huu kushindwa kushinda taji hata moja na Sunday Telegraph limeripoti kwamba, rais wa klabu hiyo, Florentino Perez amemuahidi Ancelotti Bale atapatikana.

Anatakiwa: Gareth Bale anazivutia klabu kadhaa kubwa Ulaya
Ancelotti anatarajiwa kuchukua nafasi ya
Mreno Jose Mourinho Madrid, ambaye anahamia Chelsea baada ya Mtaliano
huyo kuonyesha nia yake kuondoka Paris Saint-Germain.
Spurs inataka kumbakiza Bale na inajiamini inaweza kufanya hivyo licha ya kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Bale atakuwa na mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kabla ya kufunguliwa pazia la usajili, kujadili mustakabali wake.
Bale ameshinda tuzo za Mwanasoka Bora wa
Mwaka za PFA na ya Waandishi wa Habari za Soka na kuwa mchezaji wa
kwanza wa Spurs tangu Teddy Sheringham kufunga mabao zaidi ya 20 katika
msimu mmoja wa Ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment