MSHAMBULIAJI
Radamel Falcao anajiandaa kwenda kufanyiwa vipimo Monaco kesho kabla ya
kujiunga na klabu hiyo ya Ligue 1, Ufaransa kwa dau la Euro Milioni 60,
(sawa na Pauni Milioni 51,295,000, kwa mujibu wa taarifa nchini
Hispania.
Mshambuliaji huyo wa Colombia kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kuihama Atletico Madrid kwenda Manchester United na Chelsea.
Pamoja
na hayo, imetokea kwamba Monaco imepiga kasi na kuzipiku klabu zote na
klabu hiyo iliyorejea Ligi Kuu Ufaransa pia inataka kuwasajili nyota
wawili wa Porto, Joao Moutinho na James Rodriguez ambao kwa pamoja
watagharimu kiasi cha Pauni Milioni 60.

Ameota mbawa England: Mshambuliaji wa gharama kubwa, Radamel Falcao yuko mbioni kutua Monaco

Andondoka: Falcao amekuwa mmoja wa washambuliaji maarufu Ulaya na alikuwa akiwaniwa na Chelsea kwa muda mrefu

Kifaa: Mabao ya Mcolumbia huyo yameisaidia Atletico Madrid kutwaa Kombe la Hispania
Rais,
Dmitry Rybolovlev ana hamu sana na kuwanyakua wachezaji wawili wa
Porto, ambao ni wachezaji wenzake wa zamani Falcao aliyefunga mabao 32
katika mechi 36 msimu huu.
Kocha
wa Atletico, Diego Simeone tayari amesema mshambuliaji huyo mwenye umri
wa miaka 27 hataacha pengo akiondoka na mchezo wa leo usiku wa La Liga
dhidi ya Real Mallorca kwenye Uwanja wa Vicente Calderon unaonekana
utakuwa wa mwisho kwake Rojiblancos.
Kocha Msaidizi wa Monaco, Jean Petit ameripotiwa kuiambia Radio RCN jana: "Ndiyo, tunamtarajia Falcao na wachezaji wengine wanne au watano wa kiwango chao,"alisema.
No comments:
Post a Comment