Wednesday, May 15, 2013

REFA WA SIMBA V YANGA, SASA HAPOKEI SIMU

Saanya (katikati)...

Mwamuzi Martin Saanya aliyepewa ‘ulaji’ wa kuchezesha mechi ya watani Simba v Yanga keshokutwa Jumamosi, sasa hapokei simu hata upige kwa ‘namba ya rais’.
Saanya anayetokea Morogoro, amegoma kabisa kupokea simu yake ya kiganjani na mara nyingi imekuwa ikiita tu.
Baadhi ya wadau wameiambia Salehjembe kwamba kutopokea kwake simu ndiyo salama yake kwa sababu anataka “kuepusha” maneno.

“Unajua mechi ya Simba na Yanga ina maneno sana, mimi nimewahi kuchezesha. Hakika unakuwa huna amani hadi ipite na wakati mwingine hata ikipita hakuna amani, lawama lazima kutoka upande mmoja au pande zote,” alisema mmoja wa waamuzi wa zamani ambaye hakutaka kutajwa jina.
“Inawezekana ndiyo maana Saanya hataki kupokea simu maana akipokea tu, kuna mtu anaweza kusema alizungumza naye na mambo ni safi. Watu wengi wa mpira ni tatizo.”
Salehjembe nayo iliamua kujaribu kwa kupiga zaidi ya mara sita simu ya Saanya ambayo iliendelea kuita bila ya mafanikio.
Saanya amepewa nafasi hiyo baada ya TFF kumbadili mwamuzi Israel Mujuni Nkongo hali ambayo imefanya Simba itishie kususia mchezo huo.(SOURCE SALEH JEMBE BLOG)

No comments:

Post a Comment