![]() |
Mourinho anamatumaini kumchukua Ronaldo kutoka Real Madrid majira ya kiangazi. |
Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon amezungumzia juu ya uwezekano na mwelekeo wa Cristiano Ronaldo hapo baadaye kufuatia Jose Mourinho kuelekea Chelsea wakati huu ambapo Manchester United ikikanusha kutaka kumsajili tena nyota huyo raia wa Ureno.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 27, yuko
katikati ya vita ya kuwaniwa kwa gharama ya pauni milioni £80 baada ya
taarifa kuzidi kuzagaa kuwa mreno huyo kutokuyafurahia tena maisha
katika mji mkuu wa Hispania Madrid.
Alipoulizwa juu ya kama mreno huyo
mwenye kiwango cha juu alikuwa na furaha ndani ya Real Madrid, Calderon
amesema 'Ronaldo alisema hakuwa ni mwenye furaha tangu kuanza kwa msimu.
Nadhani mahusiano Rais wa sasa si mazuri, pengine kwasababu Rais
hakupenda mchezaji huyo aliyemrithi.

Ronaldo amefunga jumla ya magoli 55 msimu huu katika klabu ya Real Madrid.
Vilabu vitatu vya Manchester City, PSG
na
Chelsea vinatajwa kuwa na uwezo wa kumlipa mshambuliaji huyo, ambapo
Calderon anasema hadhani kama kila klabu inaweza kulipa ada hiyo ya
uhamisho kwa mchezaji huyo.
'Real Madrid wanaelekea kuzungumzia juu
ya mkataba wake na watatoa maamuzi. Ni jambo ambalo tutalijua ndani ya
wiki chache zijazo.
United walikuwa wa kwanza kujitokeza kutaka kumsajili endapo Real itaamua kumuuza ili aweze kurejea Old Trafford.
Lakini hata hivyo Mourinho, ambaye
amefanya naye kazi kwa miaka mitatu ndani ya Bernabeu amemuongeza katika
orodha yake ya awali.
Wayne Rooney, ambaye alionyesha kuitaka Chelsea, pamoja na mshambuliaji wa Napoli Edinson Cavani pia wanatakiwa na Mourinho.


Pichani juu: Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney (kushoto) na Edinson Cavani wa Napoli pia wanatakiwa na Mourinho

Abramovich anajipanga kumpa Mourinho pauni milioni £100 ya matumizi ya kiangazi.
Ronaldo ameitumikia Real Madrid kwa misimu minne lakini sasa anaonekana kukerwa na anakosa raha ndani ya klabu hiyo.
Ingawaje haitakuwa na uwezo wa
kuwashawishi washambuliaji wote watatu kujiunga na Chelsea, klabu hiyo
imedhamiria kwenda vizuri katika usajili wa kiangazi.
Mahusino ya Mourinho na Ronaldo yalikuwa
katika mashaka makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya
mshambuliaji huyo kuonekana akipiga kelele mbele ya Mourinho kwa maneno
yanayodhaniwa kuwa yalikuwa ni matusi ya ‘****
you’ baada ya kuifungia Real goli la 200.
Ronaldo inasemekana alitumia lugha ya
kireno yaliyotafririwa kama ‘I’m here, I’m here’ wakati kocha huyo akiwa
katika maandalizi ya kuondoka Hispania katika klabu ya Real baada ya
kuifundisha kwa kipindi cha miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment