na shaffih dauda
May 21st
2003 ni tarehe ambayo Jose Mourinho akiwa na kikosi cha
FC Porto alishinda ubingwa wa UEFA Cup kwa kuwafunga Celtic. Tangu
wakati huo alienda na kushinda makombe mawili ya Champions League na
makombe ya ligi katika nchi nne tofauti. Kunaweza kukawa na ubishani
mdogo tu kwamba ndiye kocha aliyetawala katika kipindi cha miaka 10
iliyopita,
japokuwa muda wake ndani ya Madrid umeisha vibaya.
2013
umekuwa mwaka wa mwisho wa zama za makocha wengi na wachezaji. Kwa
baadhi yao wamekuwa wakisifiwa kwa kazi zao ingawa kwa mtu mmoja -
Special One,wakati wake ndani ya Madrid unaangaliwa kama wakati ambao
umemfelisha Mourinho kama kocha.
Baada
ya kipigo kutoka kwa Atletico kwenye fainali ya Copa Del Rey Jose
Mourinho aliulezea msimu huu kama ndio m'bovu kuliko yote kwenye maisha
yake ya soka. Ulikuwa wa shetani kwa Madrid huku michezo miwili ikiwa
imebakia, Mourinho alitolewa nje kwa kumtusi mwamuzi akiiacha Madrid
ikiwa imeghafirika dimbani dhidi ya wapinzani wao wa jadi. Mafanikio
pekee aliyoyapata ndani ya msimu huu ni ubingwa Spanish SuperCup.
Msimu
uliopita Madrid walikuwa makini, wenye hamu ya kufanikiwa na wakiwa na
umoja katika kuuvunja utawala wa Barcelona. Pointi zao walizopata kwenye
LA LIGA zilivunja rekodi, walifunga mabao mengi na wangeweza kuzidisha
idadi hiyo kama wangekuwa makini. Wangeweza kufanikiwa zaidi msimu
uliopita kama wangeshinda kwenye penati kwenye nusu fainali ya ligi ya
mabingwa wa ulaya - kufungwa kwao usiku ule ulikuwa mwisho wa umoja wao.
ere driven, determined and importantly
together in their quest to overcome Barcelona.
Madhara
ya kutokuwa na umoja yalionekana msimu huu. Hamu ya kutaka kufanikiwa
ulaya zaidi ilizaa sumu iliyokuwa ikimtafuna Mourinho, ligi ikaonekana
haina umuhimu hivyo ndivyo atleast kiwango na matokeo yalivyokuwa
yakionyesha. Real walikuwa kwenye kiwango cha kawaida sana kwenye ligi
wakikosa nguvu na muamko. Kama mlengo ulikuwa ni UCL, basi approach
haikuwa sahihi, nguvu nyingi zilitumika mwanzoni na wakati wakielekea
mwisho ndivyo nguvu ilivyopungua. Kiwango walichoonyesha kwenye mechi
dhidi ya Manchester United na Galatasary kilikuwa cha wastani, aibu
ikawakumba kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Dortmund
waliocheza kitimu dhidi ya Madrid waliokuwa wakicheza kibinafsi
NUSU FAINALI 3 ZA CHAMPIONS LEAGUE HAYAKUWA MAFANIKIO NDANI YA MADRID
Nguvu
ya Mourinho ilianza kufifia mwaka uliopita, tabia yake ilianza kuchosha
na kutambua kwake kwamba msimu huu utakuwa wa mwisho kwake ilizidi
kufanya hali kuwa mbaya. Alianzisha vita ambazo zilikuwa ngumu kwake
kushinda na mwishowe wake zikaleta mgawanyiko kwa wachezaji na yeye
mwenyewe.
Kama
hii ilikuwa ndio plan yake ya kulazimisha kuondoka Madrid anaweza akawa
amefanikiwa. Timu yake ilikuwa imesambaratika msimu mzima na anaiacha
klabu hiyo kwenye hali mbaya. Ndio kuna wachezaji wa kiwango cha dunia
kwenye timu hii ya sasa, lakini inahitaji kuundwa upya iwe kitimu zaidi.
Kuondoka kwa Mourinho ni jambo zuri kwa pande zote
Kipigo
cha Copa Del Rey kimeonyesha kwa picha safi nini kilikuwa tatizo msimu
huu na Mourinho ndio mtu wa kulaumiwa. Ataondoka Madrid mwishoni mwa
msimu huu, na mabaya yake yamemfanya kuonekana amefeli kufanya kile
alicholetwa kufanya ndani ya Madrid. Jukumu kubwa lilikuwa kushinda
ubingwa wa Champions League ambao ameshindwa, nusu fainali 3 zinaweza
zikawa rekodi nzuri kwa timu nyingine lakini sio Madrid.
Kombe
moja la ligi ndani ya miaka 3 na moja la Copa Del Rey ni mafanikio
kidogo kwa kocha wa aina yake aliyepewa matumaini makubwa kutokana na
kauli zake mwenyewe. Mourinho ni kocha anayejijali yeye zaidi kuliko
timu yake, napenda kuwa juu ya klabu - hii inatajwa kuwa sababu mojawapo
iliyomnyima kazi Manchester United. Anakosa ujuzi au hali ya kujtaka
kujenga timu kwa malengo ya muda mrefu. Hili ndio limemwangusha ndani ya
Madrid.
BARCELONA
Ukweli
ni kwamba sababu nyingine kuu iliyomleta Mourinho Bernabeu ilikuwa ni
kuuvunja utawala wa Barcelona. Alijaribu lakini hali imerudi vilevile
sasa hivi wamerudi kwenye kivuli cha wapinzani wao. Alipowasili Santiago
Bernabeu alikumbana na kipigo kibaya cha 5-0 na matokeo yake yake mbinu
za mchezo wa Mourinho zikabadilika ndani ya Madrid.
Mbinu
zake za kucheza dhidi ya Barcelona zilibadilika kabisa na badala ya
kufanya mabadiliko kadhaa kwenye timu yake, alikiri kwamba timu yake ni
haiwezi Barca na njia pekee ya kucheza dhidi yao na kuwashinda ilikuwa
kwa mbinu chafu za vurugu na udanganyifu.Ikiwa tu angeweza kuiendeleza
timu yake kwa mfano wa Dortmund na Bayern Munich labda tayari angeweza
kuumaliza utawala wa Barcelona kwa kupata mafanikio zaidi hata kwa
kubeba kombe la ulaya.
Baada
ya majaribio kama 10 kwa mbinu zake Mourinho akaanza kufanikiwa lakini
alikuwa ameshachelewa. Barca walionyesha kuwa na mentallity na imani
kwenye aina ya mchezo wao na kuwa na mchezaji aina ya Messi waliweza
kufanya visivyowezekana pale ilipohitajika. Pamoja na vita ya umalaika
vs ushetani baina ya Mourinho dhidi ya Guardiola uliifanya El Classico
izidi kuandamwa na vituko, lakini mwisho wa siku Guardiola alimshinda
mpinzani wake.
Vita
hii ilimfanya Mourinho aonekane mkorofi mwenye mbinu chafu hata ushindi
wake ulikuwa wenye malalamiko. Huyu hakuwa kocha mwenye heshima bali
mwenye wivu na majivuno. Mourinho aliwasili Santiago Bernabeu akiwa
bingwa wa ulaya kama ilivyokuwa wakati akiwasili Chelsea ingawa muda huu
alikutana na kiboko yake ambaye hakumpata England.
Alidhalilishwa
na Guardiola, aliyekataa kucheza mchezo alioutaka Mourinho. Hivyo
ikazaliwa vita ya class vs fashion kati yao. Katika miaka iliyopita
Mourinho alionekana kama kocha kijana mnadhifu mwenye kuvaa Armain Suit
lakini bado Guardiola alimshinda hata kwenye vita hiyo. Ukweli ni kwamba
Barcelona na Guardiola walionyesha dhahiri ya ubovu wa Mourinho.
VITA BINAFSI MBELE YA MASLAHI
Vita
ya Mourinho dhidi ya Barcelona, ilipelekewa na mreno huyo kunyimwa kazi
mwaka 2008, alisahau kuweka umakini wake kwenye klabu yake
aliyoifundisha kwa miaka 3. Vita yake na Barcelona haikuharibu sifa yake
binafsi bali pia na ile ya Madrid.
Unaweza
ukajaribu kubisha kwa namna alivyoileta uimara kwenye ambao haukuwepo
miaka mingi iliyopita, lakini Pellegrini angeweza kufanikiwa zaidi ikiwa
angepewa nafasi ya kuendelea kuwa kocha baada ya msimu wake aliomaliza
na pointi 96. Pia Pellegrini asingeweza kusababisha migongano na
matatizo kwa wachezaji na klabu kwa ujumla.
Ndio
maana haikushangaza kuona wachezaji wake wenyewe wakikosana nae - pia
haikushangaza kuona wale wachezaji wanaoijua Madrid haswa kiundani
walianza kutofautiana nae. Wachezaji ambao tayari walishakuwa na medali
za ubingwa wa dunia waliambiwa wacheze mchezo ambao hawakuupenda ili
kuweza kuwashinda Barcelona. Haikuwa kama ilivyokuwa kwenye vilabu
alivyopitia huko nyuma ambapo aliweza kuwashawishi kuamini kwenye mbinu
zake. Kwa sababu tofauti na Porto, Chelsea na Inter, wachezaji wa Madrid
tayari walishakuwa washindi. Na baadhi ya wachezaji wa kihispania
walikuwa kwenye timu ambayo inasifika kwa kucheza soka safi kuliko timu
zote ulimwenguni.
Kwenye
macho yao waliona mbinu za Mourinho zilikuwa zinatofautiana na
utamaduni wa Spain na ule wa Madrid. Ugomvi wake na Ramos na Casillas
ulikuwa kielelezo tosha. Alipoteza imani ya wachezaji muhimu ndani ya
timu, matamanio ya Mourinho yalikuwa kuwadhibiti wachezaji hao ili
kuweza kutawala vizuri. Lakini hili ndio likazidisha tatizo, wachezaji
hawa haswa Casillas alikuwa mkubwa na mwenye umuhimu ndani ya klabu
kuliko Mourinho. Kama ingetakiwa mmoja aondoke baina yao basi Casillas
angebaki.
Ndio
mwanzoni alipewa rungu na akaweza kumuondoa Raul, lakini kadri siku
zilizovyokuwa zikienda ndivyo alivyozidi kugundua Casillas ni kizingiti
kikubwa katika utawala wake - na hii ni moja ya sababu zilizomuangusha
Mourinho ndani ya Madrid.
Ingekuwa
Mourinho angeweza kumtumia vizuri kipa basi angeweza kujiletea
mafanikio binafsi na ya timu lakini badala yake akaamua kuwa na vita nae
. Ukosefu wa umoja na ushirikiano ndani ya kikosi ndio sabau kuu ya
anguko la Madrid msimu huu na mtu wa kumlaumu ni Mourinho mwenyewe.
Sio "Special One" tena
Mwanaume
huyu aliyewasili mwaka 2010 akiwa bingwa wa ulaya, The Special One
anaondoka Madrid akiwa amefeli na chini ya kivuli cha kocha
aliyefanikiwa zaidi kwenye kipindi cha miaka 10 iliyopita. Swali ni - je
tumeshaona ubora wote wa Mourinho? Makocha kama Guardiola na Klopp
wanaonekana kuwa makocha wa kisasa zaidi wenye kujiheshimu. Tunashuhudia
kizazi cha makocha wapya na nina mashaka kwamba Mourinho atapata
mafanikio yoyote yatakayokaribia mafanikio aliyoyapata muongo mmoja
uliopita.
Ikiwa
atarudi Chelsea kama inavyotegemewa itadhihirika kwamba amefeli kwenye
levo ya juu, ndio alikuwa bora kwa miaka kadhaa iliyopita lakini amefeli
ndani ya Madrid na kuvionyesha vilabu kama United, Barcelona na Bayern
Munich kwamba hafai kuwa kiongozi ndani ya timu zao. Hata Man City
ambapo wafanya maamuzi ni watumishi wa zamani wa Barca inaonekana
hawataki kujihusisha nae. Ukweli ni kwamba Madrid imempotezea sifa yake
kama kocha bora kutokana na kufeli kufanya kazi kama ilivyopaswa.
No comments:
Post a Comment