Sunday, May 12, 2013

LAMPARD AVUNJA REKODI YA MABAO MENGI CHELSEA


 
Frank Lampard amefunga bao lake la 202 na 203 kwa Chelsea na kumvuka Bobby Tambling aliyekuwa anashikiria rekodi ya ufungaji wa mabao mengi katika klabu hiyo.
Pamoja na kufunga mabao hayo katika mechi ya Aston Villa na kuvunja rekodi hiyo, Lampard ameigakikishia Chelsea nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kufikisha pointi 72 ingawa Arsenal wanaonekana kutokata tama.

Baada ya mechi hiyo, Lampard alizungumza na Tambling kuhusiana na suala hilo la rekodi.
Pamoja na kuvunja rekodi ya Tambling, kiungo huyo mkongwe wa Chelsea anashikilia rekodi ya kuwa kiungo mwenye mabao mengi zadi katika Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment