Katika
Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mchujo ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya
Kombe la Shirikisho, Supastraika wa Tanzania, Mbwana Samataa, alifunga
Bao na kuisaidia TP Mazembe kuisambaratisha Liga Muculmana de Maputo kwa
Bao 4-0 katika Mechi iliyochezwa huko Lubumbashi.
Raundi
hii imezikutanisha Timu 8 zilizotolewa Raund ya Pili ya CAF CHAMPIONZ
LIGI na zile zilizoshinda Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho.
TP
Mazembe ilibwagwa nje ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Orlando Pirates ya Afrika
Kusini baada ya kufungwa Bao 3-1 huko Afrika Kusini na wao kushinda 1-0
waliporudiana Mjini Lubumbashi katika Mechi ambayo walikosa nafasi
nyingi za wazi za kupata Bao la pili ambalo lingewabakisha CHAMPIONZ
LIGI.
Bao za TP Mazembe:
-Dakika ya 16 Richard Kissi Boateng [Ghana]
-26 Given Singuluma [Zambia]
-53 Mbwana Samatta [Tanzania]
-80 Nathan Sinkala [Penati] [Zambia]
No comments:
Post a Comment