SIMBA
SC imekamilisha usajili wa kikosi cha msimu ujao kwa asilimia 80 na
ndani yake itakuwa na wachezaji wanne wa kigeni, akiwemo mshambuliaji
Moses Oloya kutoka Uganda.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia MPIRA MAENDELEO leo kwamba wamekamilisha mazungumzo na kufikia makubaliano na
Oloya, na sasa kuna kitu kimoja wanasubiri kabla ya kusaini naye
mkataba.
“Timu
ya taifa ya Uganda inakwenda Libya kucheza mechi za kufuzu za Kombe la
Dunia. Akimaliza anakwenda kwenye klabu yake kuchukua barua ya
kututhibitishia hana mkataba, ndipo tutampa chake naye asaini,”alisema HANS POP ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuhakikisha CHAMA LA WANA linatisha msimu ujao kuanzia kwenye michuano ya KAGAME.
Kiungo
huyo mshambuliaji wa The Cranes, yaani ndege aina ya Korongo
aliyezaliwa miaka 20 iliyopita anamaliza mkataba wake na Saigon Xuan
Thanh ya Vietnam Agosti mwaka huu, lakini ameamua kuuvunja kutokana na
klabu hiyo kukiuka mambo ya msingi katika mkataba huo.
Anadai
klabu hiyo haijamlipa mshahara kwa zaidi ya miezi mitatu, hivyo pekee
hiyo inahalalisha uvunjwaji wa mkataba baina yao naye kutua Msimbazi
kama mchezaji huru.
Simba ikimpata mchezaji huyo aliyekwenda Vietnam akitokea KCC ya kwao, aliyoichezea tangu 2009 hadi 2010, itakuwa imelamba dume.
Oloya
ni mchezaji mzuri kuliko Emmanuel Okwi ambaye Simba SC imemuuza Etoile
du Sahel ya Tunisia na Desemba mwaka jana, Yanga SC na Azam zote
zilijaribu kutaka kumsajili bila mafanikio.
Mwishowe
Azam ikaona bora kumsajili Brian Umony, wakati Yanga ilibanwa na nafasi
ya idadi ya wachezaji wa kigeni, lakini ikamuweka kwenye orodha ya
wachezaji inayoweza kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
Mbali
na Oyola, wachezaji wengine wa kigeni wa ndani ya Simba watakuwa
Waganda watupu, kipa Abbel Dhaira, beki Samuel Ssenkoom na kiungo Mussa
Mudde, maana yake klabu hiyo ina nafasi moja ya mchezaji wa kigeni kwa
mujibu wa kanuni.
Katika
mazoezi ya Simba yanayoendelea kwenye Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es
Salaam, chini ya kocha mpya Abdallah Athuman Seif ‘King Kibaden’
wamejitokeza wachezaji zaidi ya 20 kufanya majaribio, wakiwemo kutoka
Nigeria, DRC, Senegal, Ivory Coast na Msumbiji mbali ya wazawa.
Adeyoum
Saleh Ahmed, beki wa kushoto timu ya taifa ya Zanzibar na klabu ya
Miembeni ya Zanzibar ni kati ya wachezaji ambao wamekuwa kivutio katika
mazoezi hayo.
Tayari
Simba SC imewasajili moja kwa moja wachezaji wanne wazawa, kipa Andrew
Ntalla kutoka Kagera Sugar, beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa
Sugar, kiungo Twaha Shekuwe ‘Messi’ kutoka Coastal Union na mshambuliaji
Zahor Pazi kutoka Azam FC, aliyekuwa anacheza kwa mkopo JKT Ruvu.
No comments:
Post a Comment