BAADA ya kunyanyua Kombe la 13 la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, Sir Alex Ferguson na kocha gwiji wa Manchester United amesema alimtema Wayne Rooney kwenye kikosi kilichomenyana na Swansea City leo kwa sababu mwanasoka huyo wa kimataifa wa England ameomba kuhama timu.
Mabingwa hao wapya, walioibuka na
ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea katika mchezo huo wa mwisho wan Ferguson
nyumbani ndani ya miaka yake 27 kazini, walishuka dimbani bila
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na hawakumuweka benchi pia.
Ferguson amethibitisha Rooney
hakuhusishwa kwa sababu ameomba kuondoka, lakini amechanganyikiwa kwa
klabu kukataa kumtema mwishoni mwa msimu.
"Sifikiri
Wayne alikuwa tayari kucheza kwa sababu ameomba kuondoka,"alisema.
"Nafikiri anataka kufikiria kadiri ya mawazo yake; Nafikiri hilo ni wazo
zuri.
"Hatutamuacha aondoka. Nafikiri amechanganyikiwa sana ametolewa nje mara moja au mara mbili katika wiki chache,".
Alisema: "Tumegoma [ombi la uhamisho] - anahitaji kwenda kujifikiria juu ya hilo,".
Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 71 anaamini Rooney amechanganyikiwa kwa
kucheza kidogo msimu huu. Ferguson amekuwa akimpa nafasi mfungaji bora
wa Ligi Kuu, Robin van Persie kama mshambuliaji kiongozi na amekuwa
akimuanzisha Danny Welbeck badala ya Rooney mbele.
Mechi ambazo Rooney ameanza amekuwa akitolewa na Ferguson amemtoa mapema mara kadhaa katika wiki za karibuni.

Wakati wa kufurahia: Wayne Rooney (kulia) aliungana na mtoto wake Kai uwanjani baada ya mechi

Usumbufu: Rooney akiwa na Ferguson (kulia) baada ya kupokea Medali yake
No comments:
Post a Comment