MSHAMBULIAJI
Wayne Rooney aliyekuwa katika wiki ngumu, ameishia kwenda kujiliwaza
katika viwanja vya gofu na mchezaji mwenzake wa Manchester United,
Johnny Evans.
Huku
tetesi zikiwa zimeenea kwamba ataondoka na kuhamia Chelsea, Paris,au
Madrid, Rooney alikwenda kutuliza kichwa yake katika gofu.

Rooney katika gofu


'WR10', jezi anayovaa Manchester United.
Rooney
hakuvaa jezi uwanjani wakati United inapokea taji la ubingwa wa Ligi
Kuu kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea 2-1 Jumapili iliyopita.
Kuna
wasiwasi baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika mechi ya mwisho ya
Sir Alex Ferguson kama kocha United, huenda asipate nafasi nyingine tena
ya kutinga uzi wa Mashetani hao Wekundu.

WR10! Rooney na begi lake la gofu

Nguvu: Rooney akimuangalia Johnny Evans akipiga kipira cha gofu


Alex Ferguson akiwa Dante Stakes Day huko York


KIUNGO David Beckham amesstaafu soka akiwa na umri wa miaka 38, uamuzi ambao ameutangaza rasmi leo.
Nahodha huyo wa zamani wa England,
anayekwenda kwa jina la utani 'Mipira ya Dhahabu', atatungika daluga
zake baada ya kunyanyua taji lingine la ligi ya Ufaransa akiwa na Paris
St Germain.
Beckham ameamua kustaafu na sasa
ataelekeza muda wake mwingi kwa mkewe Victoria na watoto wake wanne,
mdogo kabisa ni Harper, mwenye miezi 21 tangu kuzaliwa.
Beckham amesema katika taarifa yake
iliyoifikia BIN ZUBEIRY leo kwamba: "Nawashukuru PSG kwa kunipa nafasi
ya kuendelea, lakini nafikiri sasa ni wakati mwafaka kumaliza, nimecheza
katika kiwango cha juu,".

Hisia: David Beckham akizungumzia kustaafu kwake soka baada ya miaka 21 

Mwisho wa zama: Beckham amesema; "Naupenda sana mchezo - Nafikiri na wakati mwafaka kuondoka'


Mtu wa wakati: David Beckham, katika
picha aliyopigwa akiwa kwenye viwanja vya mazoezi vya Paris Saint
Germain leo akitangaza kustaafu
No comments:
Post a Comment