

Sir
Alex Ferguson ameipongeza Liverpool kwa kuandaa mchezo wa jumapili kuwa
ni mchezo wa mwisho rasmi kwa mlinzi mkongwe Jamie Carragher ambapo
atapewa heshima zote za kuelekea kustaafu kwake na ambao utakuwa mchezo
wake wa mwisho.
Mlinzi huyo ataachana rasmi na soka baada ya miaka 16 ya utumishi wake akiwa ni roho ya ulinzi ya Liverpool.
Carragher,
ambaye ni mchezaji wa pili katika orodha ya wachezaji wa Liverpool
walioitumikia michezo mingi na sasa anafuata nyayo za meneja huyo
mkongwe aliyethibitisha kuacha kukalia benchi la ufundi la Manchester
United.
Ferguson
walikuwa na kikwazo cha sehemu ya ulinzi cha Liverpool ambapo mlinzi
huyo wa zamani wa England amekuwa sehemu ya ulinzi katika jumla ya
makutano 33 ya klabu hizo mbili katika kipindi cha miongo miwili
iliyopita.
Akiongea katika sehemu ya makala yake ya miaka 35 ya utumishi wake kama kocha Ferguson amesema
‘Ni mchezaji niliye mpenda sana. Alikuwa ni mchezaji anajitoa ambaye Liverpool walibahatika kuwa naye kwa miongo miwili.
‘Alikuwa
na ubora kwa miaka nenda miaka rudi. Nilimpenda. Ni mfano kwa vijana
ambao wanataka kucheza soka, alikuwa kweli mcheza soka mweledi.

Carragher atacheza mchezo wake wa mwisho wa Liverpool dhidi ya QPR Jumapili.
Wakati
huo huo imetangazwa kuwa Liverpool na QPR watampa Carragher heshima ya
kipekee atakapo chomoza katika mchezo huo wa mwisho.
No comments:
Post a Comment